Ndugu Wana Jamii, juzi nilisoma sehemu moja Bw. Ryoba yule Mhadhili kutoka UDSM nadhani kwenye masuala ya Habari na pia ni Mwenyekiti wa Asasi isiyokuwa ya Kiserikali ya Mashariki na Kusini mwa Afrika inayohusu masuala ya Habari, akilalamika kwamba kuna mwanadishi mmoja kaandika kwamba "yawezekana watu wa Musoma bado ustaarabu kwao ni mdogo" lakini pia nilimsoma Bw. Kabwe akimuunga Mkono Ryoba kwa kusema sisi Watanzania tuna tabia ya kuhukumu bila hata ya kuwa na habari kamili.
Wote walikuwa wanampinga mwandishi alyesema Musoma USTAARABU kwao bado upo nyuma sana - suala ni mauaji ya watu 17.
Mimi nimeandika kwamba, hivi huyu Bw. Ryoba na Mhe. Kabwe wanataka mtu ufanye utafiti wa namna gani au uwe na Elimu ya namna gani au uwe na akili ya namna gani ili uje watu wa Mkoa wa Mara HAWANA USTAARABU katika kudhamini uhai wa watu wengine.
Mifano ni mingi, niliwahi kwenye Tarime na Kiongozi mmoja, katika ziara ile tulifanya Mkutano na Jamii za kule zainazopigana, majibu waliyokuwa wanayatoa utajua kabisa kwamba hawa jamaa ama AKILI zao zinatatizo au bado wanaishi ile DUNIA YA 1800 ambayo majadiliano ni KOSA KABISA. Walyanchoka, wanayabasi n.k wanachinjana na kuchomeana nyumba. Wengine ni Kabila moja la Kikurya au Kijaluo lakini tofauti ua Ukoo inawanya kuuana kwa mapanga na Mikuki.
Katika Mkutano huo walikuja na mapanga yao na mikuki na mishale.
Hivi nani hajuwi kuwa kutokana na hali mbaya ya usalama wa kuuana Serikali imeigeuza Wilaya ya Tarime kuwa Mkoa wa Kipolisi? hivi dunia ya leo bado watu wanachinjana kwa kosa la kuchukiana? unachinja familia nzima.
Mkoa wa Mara wanachofanya kuna tofauti gani na mauji ya halaiki kule Rwanda au Burundi? wa kwa sababu wapo Tanzania?
Mifano ni mingi. Nilipata bahati ya kuongea na Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Issa Machibya kabla hajahashwa kule, anasema Mkoa wa Mara ni hatari ZAIDI kuliko Mkoa wowote wa Tanzania kwa sababu ya mauaji ya wenyewe kwa wenyewe. (NADHANI SERIKALI IANZISHE MAHAKAMA MAALUM YA MAUAJI YA MKOA WA MARA).
Niliwahi kwenda Wilaya ya Serikali kufanya ukaguzi wa Hesabu kwenye Halmashauri ya Wilaya, ilipofika usiku saa 2 nilitoka Guest niliyofikia nikawa naenda kutafuta chakula, kulikuwa na giza kidogo, nilimuona mmoja wa Wahasibu wa Halmashauri tulikuwa tunapishana anakwenda ninapotoka na nina kwenda anapotoka, nikamuita jina na kumwambia habari za usiku, lakini jamaa hakuitikia kabisa.
Kesho yake asubuhi nilumuuliza mbona jana usiku nilikusalimia tulipokutana hukuitikia? akasema unajua ndugu yangu huku Serengeti na Musoma kwa ujumla huwa ahutuikii salama usiku kwa sababu pengine kuna mbaya wako ameshika panga anakuita jina na kukusalimia ukiitikia tu anajua ndiyo wewe anakucharanga mapanga.
Hebu kumbuka yule mwanamama aliyepichwa na Mumewe na mchi wa kutwangia mahindi kwenye miguu hali iliyopekelea miguu yake kukatwa, huo bado utauita ustaarabu.
Nendeni Mara mkawaulize Polisi kwa hali ya UPOLE kabiwa watakuleza namna kesi za mauaji zinavyokosa mashahidi kwa sababu mtu yeyote atakayejitokeza kutoa ushahidi kichwa chake na familia yake vitakatwa kwa mapanga.
Hebu kumbuka ni miezi michache iliyopita huko huko Musoma kuna habari ilisema Bw. Mmoja amemuua Mke wake, mtoto wake wa miaka 2, wazazi wote wawili wa Mke wake, kisa Mke kamkimbia na kurudi kwao kwa kile Mwanamke alichosema kipigo cha kila siku kutoka kwa Mumewe.
Bado mnataka tuamini kwamba watu wa Musoma ni WASTAARABU kwenye mwili wa wenzao?
Bado mnataka tusiwalaumu?