unajua nadhani Jimbo la Nyamagana is becoming more tempting..
.
Kwa Tarime, kuna tatizo, ila pia ni kweli gap kati ya wenye nacho na wasionacho imezidi kukuwa siku hadi siku, itafika wakati wasio nacho, watakata tamaa na kuamua kuwanyang'anya wenye nacho ili wagawane.
Oh Lord... si nilisikia wameagiza jeshi kuhamia kabisa huko!?
Jamii ndiyo ilaumiwe kwa kuwekeana visasi visivyokwisha. Serikali itaweka jeshi katika kila kaya jamani ????
,
Tena nadhani ni Tarime, sikumbuki vizuri ni Musoma wapi, kama ni Tarime, huyu DC, Frank Uhahula, kiongozi mstaafu wa Chipukizi nwa CCM akishirikiano na OCD, anachanganya siasa na uongozi kwa kuwachonganisha wana Tarime kuwa fujo zote, mauaji ya koo na wizi wa mifugo vinatokea kwa sababu wameichagua Chadema.
Kwenye kikao cha baraza la madiwani last week, walimfukuza kwenye kikao, wakazuiliwa na kanuni, ili walimpaka sana, na jamaa akajibu mapigo kwa lugha ya ubabe, kuwa yeye anafuata taratibu, sheria na kanuni.
Walimsifu Kamanda Tosi, kikosi chake ndicho angalau kinafanyan kazi bila kuchanganya na siasa.
Hiyo wilaya iamishiwe Kenya,huku hapawafai kabisa!Tarime kuna nini? Naogopa hali hii inayoendelea kutokea Tarime isipozuiliwa na kukemewa kwa nguvu na kila mmoja wetu hizi chuki zinaweza kusambaa nchi nzima, ukizingatiwa hali ilivyo nchini walala hoi wengi wamelowa petrol wanahitaji njiti moja tu ya kiberiti kuanza kuteketezana kati walio nacho na wasio nacho!!
Hiyo hapo nyeusi si kweli kabisa na ni ushabiki unaotakiwa kutopewa nafasi. Watu wenye mtazamo wa namna hii ama waandishi wa habari wa namna hii sijui tuwaite je?
Kaangalie historia yako upya? je mapigano hayo hayakuwepo hata wakati wa chama kimoja?
Angalia makabila ya huko utakuta na Kenya makabila hayo yapo , na tena kaangalie mapigano yaliyo mipakani ya kabila kati ya kenya na uganda, kati ya kenya na somalia kati ya kenya na sudani kati ya kenya na ethiopia. Na je huko nako wameichagua CHADEMA.?
Mimi nafikiri njia sahihi ni kuacha uzushi nafikiri itakuwa njia sahihi na nguzo mathubuti ya kuindoa ccm.
Ninakwenda huko inaonekana huyu Mmarekani i mean Masha hana jipya,kanda ya ziwa ndiko anakotoka lakini kanda ya ziwa ndiko kwenye kila aina ya mauaji anzia Maalbino, Bibi vikongwe,Mauaji ya koo ujambazi na uhujumu uchumi unaofanywa na wahindi pale Mwanza mjini.Imetosha kwa Masha ni wakati wa wazawa kuwatumikia wazawa.unajua nadhani Jimbo la Nyamagana is becoming more tempting..
Yego Poti,
You are missing the point.
Suala la kuchaguliwa chadema sio maneno ya Pasco bali ni nukuu ya salam za mkuu wa wilaya ya tarime Frank Uhahula.Aliyasema maneno hayo akitoa salam siku ya maadhimisho ya miaka 33 ya ccm, na suala hilo liliibuliwa kwenye kikao cha baraza la madiwani.
Kwahiyo na wewe usitumie mahaba yako kwa ccm kutaka kutudanganya. Tunajua jinsi ccm mnavyotumia mwanya wa tofauti zilizopo kati ya koo za wakurya kujitafutia umaarufu wa bei nafuu. Tunajua mapigano ya tarime yangeweza kukomeshwa kama sio uchochezi unaoendelea kufanywa na na ccm. Kamanda massawe yuko busy kuchoma moto mashamba ya bangi lakini hafanyi lolote la maana kwa ajili ya kulinda usalama wa raia.Tunajua kuwa mmemleta massawe tarime ili kuwasaidia kuiba kura katika uchaguzi mkuu wa octber 2010 lakini jambo moja liko wazi, watu wa tarime watafanya uamuzi wao na kuhakikisha chaguo lao ndiye anakuwa muwakilishi wao.
Nsokili mosani!!!
Tatizo la ujambazi sio geni tangu walipokubali kuhujumu uchumi wa Tanzania na tatizo sio Masha peke yake tatizo ni Chama Cha Majambazi na serikali inayoongozwa na Jakaya Kikwete - kwishnei.
Kaka haya mauaji hayahusiani kabisa na ujambazi ni ujinga na ushenzi wa binaadam wa mkoa wa Mara, maana haya mambo yanatokea huko tu na si mahala popote pale Tanzania, ingelikua kuna possibility ya kuuza mkoa basi MARA unatakiwa kuuzwa tena kwa mkopo kama Michael Owen.. MKOA WA MARA UNATIA AIBU SAAAAAAAAANA WATANZANIA, najuuta kuwa Mtanzania because of this region