16 Wauwawa kwa Kucharangwa Mapanga Usiku wa Manane-Musoma

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
26,270
Likes
26,178
Points
280

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
26,270 26,178 280
Watu 17 wa Ukoo Mmoja wakiwemo watoto wadogo, wameuwawa kwa kucharangwa mapanga usiku wa manane wa kuamkia leo huko Musoma.

Kwa mujibu wa Radio One Breaking News asubuhi hii, mauaji hayo yanahusishwa na tukio la kulipiza kisasi lililohusisha watu wa koo moja dhidi ya nyingine!.

Marehemu watazikwa kesho!.

Very sad!.
Update 1

Watu 17 wauawa Musoma
Imeandikwa na Basil Msongo; Tarehe: 16th February 2010 @ 13:17 Imesomwa na watu: 419; Jumla ya maoni: 1

WATU 17 wakiwemo watoto wanane wameuawa usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha Buhare, nje kidogo ya mji wa Musoma mkoani Mara.

Watu waliouawa ni wa familia tatu, wanane kati ya hao ni wa familia moja akiwemo mume, mke, na watu wengine sita.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara, Robert Boaz, amezitaja familia zilizokumbwa na maafa hayo kuwa ni za Kawawa Nyarukembe iliyopoteza watu wanane, Morice Mgaya imepoteza watu sita, na familia ya Mgaya Nyarukembe imepoteza watu watatu akiwemo mke wa mwenye nyumba.

Kamanda Boaz amesema, watu wasiofahamika walizivamia familia hizo saa sita usiku, wakavunja milango ya nyumba na kuwashambulia wanafamilia kwa silaha zenye ncha kali.
Miongoni mwa waliouawa ni wanawake 11, wanaume sita, watano kati ya marehemu ni watoto wa kike, na watatu ni watoto wa kiume.

Polisi wanahisi kuwa mauaji hayo yamesababishwa na kisasi.
 

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
26,270
Likes
26,178
Points
280

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
26,270 26,178 280
Oh Lord... si nilisikia wameagiza jeshi kuhamia kabisa huko!?
,
Tena nadhani ni Tarime, sikumbuki vizuri ni Musoma wapi, kama ni Tarime, huyu DC, Frank Uhahula, kiongozi mstaafu wa Chipukizi nwa CCM akishirikiano na OCD, anachanganya siasa na uongozi kwa kuwachonganisha wana Tarime kuwa fujo zote, mauaji ya koo na wizi wa mifugo vinatokea kwa sababu wameichagua Chadema.

Kwenye kikao cha baraza la madiwani last week, walimfukuza kwenye kikao, wakazuiliwa na kanuni, ili walimpaka sana, na jamaa akajibu mapigo kwa lugha ya ubabe, kuwa yeye anafuata taratibu, sheria na kanuni.

Walimsifu Kamanda Tosi, kikosi chake ndicho angalau kinafanyan kazi bila kuchanganya na siasa.
 

Brooklyn

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2009
Messages
1,460
Likes
51
Points
145

Brooklyn

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2009
1,460 51 145
Tarime kuna nini? Naogopa hali hii inayoendelea kutokea Tarime isipozuiliwa na kukemewa kwa nguvu na kila mmoja wetu hizi chuki zinaweza kusambaa nchi nzima, ukizingatiwa hali ilivyo nchini walala hoi wengi wamelowa petrol wanahitaji njiti moja tu ya kiberiti kuanza kuteketezana kati walio nacho na wasio nacho!!
 

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
26,270
Likes
26,178
Points
280

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
26,270 26,178 280
Tarime kuna nini? Naogopa hali hii inayoendelea kutokea Tarime isipozuiliwa na kukemewa kwa nguvu na kila mmoja wetu hizi chuki zinaweza kusambaa nchi nzima, ukizingatiwa hali ilivyo nchini wananchi wengi wamelowa petrol wanahitaji njiti moja tu ya kiberiti kuanza kuteketezana kati walio nacho na wasio nacho!!
.
Kwa Tarime, kuna tatizo, ila pia ni kweli gap kati ya wenye nacho na wasionacho imezidi kukuwa siku hadi siku, itafika wakati wasio nacho, watakata tamaa na kuamua kuwanyang'anya wenye nacho ili wagawane.
 

Kimbweka

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2009
Messages
8,609
Likes
54
Points
145

Kimbweka

JF-Expert Member
Joined Jul 16, 2009
8,609 54 145
,
Tena nadhani ni Tarime, sikumbuki vizuri ni Musoma wapi, kama ni Tarime, huyu DC, Frank Uhahula, kiongozi mstaafu wa Chipukizi nwa CCM akishirikiano na OCD, anachanganya siasa na uongozi kwa kuwachonganisha wana Tarime kuwa fujo zote, mauaji ya koo na wizi wa mifugo vinatokea kwa sababu wameichagua Chadema.

Kwenye kikao cha baraza la madiwani last week, walimfukuza kwenye kikao, wakazuiliwa na kanuni, ili walimpaka sana, na jamaa akajibu mapigo kwa lugha ya ubabe, kuwa yeye anafuata taratibu, sheria na kanuni.

Walimsifu Kamanda Tosi, kikosi chake ndicho angalau kinafanyan kazi bila kuchanganya na siasa.
Musoma ni musoma! na Tarime ni Tarime
 

Mzee Kibiongo

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2008
Messages
241
Likes
0
Points
0

Mzee Kibiongo

JF-Expert Member
Joined Jun 18, 2008
241 0 0
Bujibuji

Nimekusoma. Ni Musoma, siyo Tarime, tusichanganye mambo, kasomeni jiografia yenu vizuri. Serikali hapa inalaumiwa vipi, sioni cha kuilaumu serikali. Jamii ndiyo ilaumiwe kwa kuwekeana visasi visivyokwisha. Serikali itaweka jeshi katika kila kaya jamani ????
 

Malafyale

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2008
Messages
11,837
Likes
4,461
Points
280

Malafyale

JF-Expert Member
Joined Aug 11, 2008
11,837 4,461 280
Bujibuji

Nimekusoma. Ni Musoma, siyo Tarime, tusichanganye mambo, kasomeni jiografia yenu vizuri. Serikali hapa inalaumiwa vipi, sioni cha kuilaumu serikali. Jamii ndiyo ilaumiwe kwa kuwekeana visasi visivyokwisha. Serikali itaweka jeshi katika kila kaya jamani ????
Mzee Kibiongo,no matter what kama kumetokea vifo vya watu wengi serikali iliyopo madarakani inabeba lawama zote.Serikali isiyoweza kuwalinda watu wake haifai kuwepo madarakani.

Serikali ya Mkoa wa Mara inatakiwa iwe na mabaraza ya kudumu ya usuluhishi kati ya koo zinazopingana ambazo zinajulikana lkn hamna jitihadi zozote za kumaliza uhasama huo

Ipo siku Tanzania itaingia kwenye mzozo maana sasa kila siku ni mauaji huko Musoma na Tarime,kwingine kusikotulia ni kule Kilosa na kule Ngorongoro ambako pia kuna uhasama wa kiukoo hasa kati ya koo za wafugaji na wakulima!

Serikali iingilie kati masuala haya ya uhasama wa kiukoo na kuwapatanisha wanaopingana,tukiacha mambo haya tutakuwa kama Somalia!
 

Bigirita

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Messages
15,060
Likes
1,740
Points
280

Bigirita

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2007
15,060 1,740 280
jumla ya vifo vya raia wasio na hatia ndani ya miezi miwili ni 30.
16 - Musoma, 14 Ukerewe.
hapo bado wale walioitwa majambazi - polisi wakiuwa watu wanawaita majambazi.

RIP raia mliyofikwa na mauti.
 

Forum statistics

Threads 1,203,485
Members 456,791
Posts 28,115,236