Jeshi la Kizayuni limeua kwa halaiki jamaa 22 wa familia ya ripota wa Aljazeera

Malaria 2

JF-Expert Member
Oct 17, 2023
2,648
3,938

Dec 07, 2023 07:06 UTC

Televisheni ya Al Jazeera ya Qatar imelaani mauaji ya familia ya mmoja wa waandishi wake wa habari katika mashambulizi yaliyofanywa na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel huko Gaza.

Katika shambulio lililofanywa na utawala wa Kizayuni katika kambi ya Jabalia iliyoko kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, watu 22, akiwemo baba na kaka kadhaa wa ripota wa Al Jazeera Momin Al-Sharafi wameuawa shahidi pamoja na watoto wao.

Kwa mujibu wa Al-Jazeera, ripota wa chaneli hiyo ya televisheni Momin Al-Sharafi ametaka jeshi la Kizayuni lifunguliwe mashtaka kwa uhalifu dhidi ya waandishi wa habari na raia wa Gaza.

Baadhi ya waandishi wa habari waliouawa shahidi Gaza
Al-Sharafi ameongeza kuwa: chaneli hiyo ya habari itachukua hatua zinazohitajika kisheria katika taasisi husika ili kuwafuatilia na kuwafungulia mashtaka maafisa wa Kizayuni waliohusika na jinai hiyo ya kutisha.

Akisimulia jinai hiyo waliyofanyiwa watu wa familia yake, ripota huyo wa Al Jazeera amesema: askari wa utawala wa Kizayuni walidondosha pipa la mada za miripuko juu ya nyumba waliyokuwemo ndani yake watu wa familia yake.

Mbali na familia za waandishi wa habari, utawala dhalimu wa Kizayuni umeshaua pia makumi ya waandishi wa habari tangu ulipoanzisha mashambulio ya kinyama dhidi ya Ukanda wa Gaza tarehe 7 Oktoba mwaka huu.

Kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni, wanahabari wasiopungua 73 wameuawa shahidi ndani ya kipindi cha siku 57 za vita vya Gaza.

Wakati huohuo Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza katika ripoti yake kuwa zaidi ya watu 16,000 wameuawa shahidi katika mashambulizi ya kinyama ya Israel dhidi ya Gaza tangu Oktoba 7, na takribani watu 41,000 wamejeruhiwa huku wengine 1,000 wakiwa hawajulikani waliko.
 
Unaharibu pale unapoandika hao waandishi wamekufa Shahid sijui Shaheen!

Hayo mauaji unakuwa umeshayapa sura nyingine,na pengine bahadhi ya watu wanaweza kutumia kigezo hicho kuyahalalisha!

Hata aljazeela pamoja na mahaba Yao kwa hamas hawadhubutu kamwe kulitumia Hilo neno Shaheen kwenye tukio kama Hilo!
 
Mimi kinachoniuma zaidi ni hiki, ilikuwaje Hamas kuwapiga wazayuni wakati huo huo wanajua hawana uwezo wa kukabiliana nao?

Ila duniani bhana, mwafrica atabakia vile vile, mwarabu naye vilele, halikadharika mzungu naye vilevile
 
Usiye muweza akikupiga haina maana kwamba usijiteteee

Ukikaa tu si ndio atakuua kabisa ama atazidi kukufanya atakavyo

Hamas kundi teule kabisa kabisa
 
Asante kwa Bandiko la Kimataifa Mkuu.

HII SIO SAWA.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Mimi kinachoniuma zaidi ni hiki, ilikuwaje Hamas kuwapiga wazayuni wakati huo huo wanajua hawana uwezo wa kukabiliana nao?

Ila duniani bhana, mwafrica atabakia vile vile, mwarabu naye vilele, halikadharika mzungu naye vilevile
Angalau umeongea point kubwa Sana ... waafrica tutabakia hivihivi na waarabu nao wataendelea kuwa wabishi na kuuwawa kilasiku
 
Dec 07, 2023 07:06 UTC

Televisheni ya Al Jazeera ya Qatar imelaani mauaji ya familia ya mmoja wa waandishi wake wa habari katika mashambulizi yaliyofanywa na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel huko Gaza.

Katika shambulio lililofanywa na utawala wa Kizayuni katika kambi ya Jabalia iliyoko kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, watu 22, akiwemo baba na kaka kadhaa wa ripota wa Al Jazeera Momin Al-Sharafi wameuawa shahidi pamoja na watoto wao.

Kwa mujibu wa Al-Jazeera, ripota wa chaneli hiyo ya televisheni Momin Al-Sharafi ametaka jeshi la Kizayuni lifunguliwe mashtaka kwa uhalifu dhidi ya waandishi wa habari na raia wa Gaza.

Baadhi ya waandishi wa habari waliouawa shahidi Gaza
Al-Sharafi ameongeza kuwa: chaneli hiyo ya habari itachukua hatua zinazohitajika kisheria katika taasisi husika ili kuwafuatilia na kuwafungulia mashtaka maafisa wa Kizayuni waliohusika na jinai hiyo ya kutisha.

Akisimulia jinai hiyo waliyofanyiwa watu wa familia yake, ripota huyo wa Al Jazeera amesema: askari wa utawala wa Kizayuni walidondosha pipa la mada za miripuko juu ya nyumba waliyokuwemo ndani yake watu wa familia yake.

Mbali na familia za waandishi wa habari, utawala dhalimu wa Kizayuni umeshaua pia makumi ya waandishi wa habari tangu ulipoanzisha mashambulio ya kinyama dhidi ya Ukanda wa Gaza tarehe 7 Oktoba mwaka huu.

Kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni, wanahabari wasiopungua 73 wameuawa shahidi ndani ya kipindi cha siku 57 za vita vya Gaza.

Wakati huohuo Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza katika ripoti yake kuwa zaidi ya watu 16,000 wameuawa shahidi katika mashambulizi ya kinyama ya Israel dhidi ya Gaza tangu Oktoba 7, na takribani watu 41,000 wamejeruhiwa huku wengine 1,000 wakiwa hawajulikani waliko.
Si ndo aandike vzr Ili auze habari?

Bila hivyo ataandika Nini?
 
Wakati Mujahidden wanatangaziwa waondoke maeneo husika ambayo yatalengwa walijua ni utani?Kwanini wagaza waruhusu magaidi kuweka miundombinu ya kigaidi kwenye makazi yao?
Sasa wanatafuta huruma ya dunia kwa ajili ya ugomvi ulioanzishwa na magaidi wa Hamas!
 
Hakuna anaetafta huruma
Hamas kundi teule
 
Back
Top Bottom