15 Julai, 2021; Hayati Magufuli atakumbukwa kwa kasi sana na watu wa kada zote

2019

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
2,982
4,457
Kwa kweli nisiwe mnafiki. Niliacha kupenda siasa toka baadhi ya wapinzani kuanza kuunga mkono juhudi za JPM. Marufuku ya siasa ikachangia pia. Utendaji wa hayati nao nikaupenda.

Kilichonifanya nisimpende Magufuli baadae ni hali ya mgawanyiko uliokuwa unaendelea nchini.

Haya ni Rais wetu JPM katangulia wapo waliofurahi na wapo waliosikitika pia.

Baada ya serikali ya awamu ya sita kuchukua hatamu na kuanza kufungulia mambo mengi yalifungwa na kurekebisha uhusiano na majirani, wapinzani, wafanyabishara na wafanyakazi kuongezewa mishahara,nchi ilikuwa kama umepata uhuru toka kwa mkoloni mweusi. Mama akapendwa na watu wote bila kuangalia itikadi yao.

Mara baada ya siku 100 kufika kauli yake kuhusu wapinzani na katiba mpya ikawatisha baadhi ya wananchi. Lakini bado hakupoteza mvuto.

BAJETI MPYA YA 2021-2022 YAMWARIBIA
Hapa ni lazima Hayati Magufuli akumbukwe na wote sababu alidaiwa kuwajali wanyonge zaidi kuliko matajiri. Bajeti iliyopitishwa na waziri wa fedha Mwigulu Lameck Nchemba ndio mtihani wa pili kwa Rais SSH baada ya dai la katiba mpya.

Huenda akaponzwa na waziri wa fedha lakini atabeba lawama yeye sababu yeye ndie alimteua na anaweza pia kumuwajibisha.

Je, kwa mabadiliko haya 2025 atatoboa?

USHAURI WANGU KWAKE
Pamoja na miradi mikubwa aliyokuwa amefanya mtangulizi wake haya maisha hayakuepo? Je kweli serikali imekosa chanzo kingine cha kuongeza mapata badala ya huduma zinazotumiwa zaidi na wananchi wa kawaida? Kwanini wasingebana kwenye vitu vya anasa kama alivyofanya Magufuli?

Je, ni Serikali kukamua wananchi kama njia ya kujiongezea mapato? Hakuna rasilimali zinazoweza kutumiwa kuiongezea serikali mapato?
 
Kuna mbunge mpumbavu alijisifu bungeni akisema bajeti yake kwa mwezi kwa ajili ya vocha ni 50k lakini mimi mwananchi wa kawaida bajeti yangu ya mwezi kwa ajili ya vocha ni 1k, nikipata sms za mwezi ndo imetoka hiyooooooo mpaka mwezi ujao na bado nikatwe kodi

Kmmke yule mbunge.
 
Atakumbukwa kwa kufuta FAO LA KUJITOA NSSF
Mwaka huu niliona watu wanashangilia kodi kutoka 9 to 8 wakati jamaa alipunguza toka 11 to 9%, last year, ukweli jamaa alibalance mambo, sasa kwa hali hii ndg unaona kawaida tu?

Gharama kuongezeka kiasi hiki ni jambo la kawaida?

Petroleum wameongeza kodi wakati ndio source ya kila kitu tutegemee nini hapo.

Wamekuja na eneo la miamala ya simu, najiuliza sana, hii burden itabebekaje kwenye jamii???

Ukweli walipaswa kufikiri vinginevyo, Magufuli kwa mambo yaliyokuwa yanagusa jamii namna hii hakuwa akiyaridhia kbs....

Tunamkumbuka mpaka kesho
 
Mpaka mkome!

Wakati Mwigulu anasoma bajeti ya kuongeza kodi kule bungeni mambo yalikuwa hivi hapa jf:

Uzi wa bajeti ulikuwa na replays 90

Uzi wa Sabaya ulikuwa na replays elfu 1 na zaidi

Uzi wa kusaini petition ya kumtoa Diamond kwenye tuzo za bet ulikuwa na replays 800 na zaid.

Watz hawajawahi kuwa serious na hata hili litapita tu
 
Mm sitokaa nimkumbuke mshamba, mento yule (according to Diallo), mtekaji, mtukanaji, muuaji mkubwa yule. Never on the Earth!
Mtu mwenyewe wewe una faida gani sasa si bora umfuate Lisu tu,?
Screenshot_20210624-223642.jpg
 
Mwamba! Dah!! Hatuko naye tena.

Mara ya mwisho nilikutana naye wakati akitokea Mbezi stand kwenda kupumzika, alinambia maneno matano sitayasahau maskini!

Kwa mara ya kwanza alikuwa na hofu nyingi, nikamuuliza mzee are you okay akajibu '.......kazi ya kujenga nchi hasa hapa kwetu Afrika kuna changamoto nyingi sana, nitaktafta kesho jioni nikitoka Kurasini tuongee.....'

Ndo ilikuwa mwisho,byee mwamba bye tumaini.

Wacha tuendee na Samia..
 
Atakumbukwa kwa
1) Kuwanyima watumishi nyongeza ya mishahara na madaraja kwa miaka kibao
2) Kuwanyima watumishi wa umma haki ya kuhama
3) Kuwakatalia wanufaika wa bodi ya mikopo kuwaondolea VRF
4) Kwa ukabila aliokuwa anaanza kupandikiza
5) Kwa chuki za kisiasa zilizokuwa zimeanza kushamiri. Apumzike kwa amani Magufuli.
=Kwa hayo hatuta msahau
Mh Samia ni zaidi ya kijito cha maji jangwani, ametufuta machozi na kuanza kutuondolea makovu mioyoni.
 
Back
Top Bottom