1.5Bilion zatakiwa kufukia mashimo ya dhahabu.


PakaJimmy

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Messages
16,231
Likes
351
Points
180
PakaJimmy

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2009
16,231 351 180
SERIKALI itatakiwa kutumia Dola za Marekani 1.1 milioni sawa na zaidi ya Sh1.5 bilioni kutekeleza mpango wake wa kufukia mashimo ya mgodi wa Buhemba ulioko Bunda mkoani Mara.


Mgodi huo ambao tayari umesitishwa uchimbaji wake, utatakiwa kugharimu kiasi hicho cha fedha kwa ajili kuyaweka mazingira yake katika hali ya usalama.


Gharama hizo pia zitatokana na ukweli kwamba baadhi ya kampuni za uchimbaji mkubwa wa madini, kutoweka dhamana kwa serikali kugharamia shughuli za kukarabati mazingira.


Ripoti ya hali ya mazingira ya mgodi huo iliyotolewa wiki hii jijini Dar es Salaam na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA) kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, imesema mpango wa kufunga mgodi huo haukutekelezwa ipasavyo.


"TMAA ilifanya ukaguzi wa mazingira wa mgodi uliofungwa wa Buhemba na kubaini kuwa maeneo ya mgodi huo yameachwa katika hali hatarishi," ilisema sehemu ya ripoti hiyo na kuongeza;


"Hii inatokana na ukweli kwamba mpango mzima wa kufunga mgodi haukutekelezwa ipasavyo. Inakadiriwa kuwa kiasi cha Dola 1.1 milioni za Marekani, kinahitajika kutekeleza mpango wa kufukia mashimo ya mgodi huo.

TMAA imewasilisha taarifa ya ukaguzi ya mgodi huo kwa mamlaka husika kwa hatua zaidi."


Hata hivyo ripoti hiyo imebaini kuwa baadhi ya migodi pia haitekelezi ipasavyo mpango wa usimamizi na utunzaji wa mazingira uliopitishwa na serikali.


"Huu ni ukiukwaji wa masharti ya leseni. TMAA inaendelea kushirikiana na vyombo vingine vya serikali hususan Baraza la Usimamizi wa Mazingira (Nemc), kuhakikisha kasoro zilizoonekana wakati wa ukaguzi zinarekebishwa," imesema ripoti hiyo ya uchunguzi iliyofanywa kuanzia Agosti, 2007 hadi Desemba 2009 .

Katika hatua nyingine TMAA imepanga kukagua shughuli za utunzaji wa mazingira katika migodi yote mikubwa, ya kati na baadhi ya migodi ya wachimbaji wadogo katika kipindi cha mwaka 2010.

\source:http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=17366
 
kilemi

kilemi

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2009
Messages
524
Likes
6
Points
35
kilemi

kilemi

JF-Expert Member
Joined Mar 13, 2009
524 6 35
Walipata faida kiasi gani kwenye hayo machimbo? Au nayo ni "usalama wa taifa"?
 
PakaJimmy

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Messages
16,231
Likes
351
Points
180
PakaJimmy

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2009
16,231 351 180
Gharama hizo pia zitatokana na ukweli kwamba baadhi ya kampuni za uchimbaji mkubwa wa madini, kutoweka dhamana kwa serikali kugharamia shughuli za kukarabati mazingira.
Hii inaonyesha wazi watia saini mikataba wasivyosoma mikataba hii, na ku'rush kuisaini bila kuelewa ndani kunani...huh!..shame on us!


Ripoti ya hali ya mazingira ya mgodi huo iliyotolewa wiki hii jijini Dar es Salaam na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA) kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, imesema mpango wa kufunga mgodi huo haukutekelezwa ipasavyo.
My genitals!....hee!!

Hivi ni mambo ya kusema kwa watu haya, aibu kubwa hivi?
nI NANI ALIYEPASWA kutekeleza vyema..na huyo mtu amekufa lini?...na amezikwa wapi?...kama ni mzima ameshikwa lini?...amefungwa gereza gani? Na kama hajashikwa anasubiri nini mtaani kama si kutumalizia hewa??..huh!
 
J

Jasusi

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2006
Messages
11,505
Likes
238
Points
160
J

Jasusi

JF-Expert Member
Joined May 5, 2006
11,505 238 160
Niliwahi kutembelea mji wa Victoria, Canada wakati fulani. Enzi za zamani kulikuwa na machimbo ya madini pale, sikumbuki kama ni mkaa wa mawe au madini gani. Lakini ulikuwa ni wajibu wa wachimbaji kufukia hayo mashimo na sasa kumejengwa bustani maridadi kabisa ya maua na kazi yote ilifanywa na kampuni iliyofaidika na machimbo hayo.
 

Forum statistics

Threads 1,250,869
Members 481,514
Posts 29,748,860