zitto kabwe

Zitto Zuberi Ruyagwa Kabwe (Zitto Kabwe)
Zitto Zuberi Ruyagwa Kabwe, maarufu kama Zitto Kabwe, ni mwanasiasa kutoka Tanzania kutoka chama cha ACT-Wazalendo. Zitto aliwahi kuwa mwanachama wa Chama Demokrasia na Mendeleo (CHADEMA) toka mwaka 1992 mpaka 2015 alipoachana na chama hicho.

Zitto ameshika nafasi ya Kiongozi wa Chama ACT-Wazalendo kwa miaka 9, mpaka March 2024 ambapo nafasi hiyo imechukuliwa na Dorothy Semu. Amewahi kuwa Mbunge wa Tanzania kwa vipindi viwili kuanzia 2005 mpaka 2015 akiwakilisha Jimbo la Kigoma Kaskazini.
  1. GE2025 Zitto Kabwe: Mkinichagua bei ya Simenti itashuka Kigoma

    Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Mjini kupitia Chama cha ACT- Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe amewaambia wanakigoma wakimchagua kuwa Mbunge atashusha bei ya Simenti ambayo inazalishwa katika Mkoa huo kutokana na bidhaa hiyo kuuzwa bei sawa na Simenti inayotoka Dar es salaam. Zitto Kabwe amesema...
  2. GE2025 Zitto nyumba kwa nyumba kuomba kura kata ya Businde

    Mgombea Ubunge Jimbo la Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akiomba kura wakati wa kampeni yake ya nyumba kwa nyumba iliyofanyika kwenye kata ya Businde jimboni hapo, mkoani Kigoma, Septemba 23, 2025. Zitto aliambatana na viongozi na wanachama wa chama hicho katika zoezi hilo...
  3. GE2025 Zitto: Aahidi kutatua changamoto ya Ardhi

    Mgombea ubunge Kwa tiketi ya chama Cha ACT Wazalendo Jimbo la Kigoma Mjini Zitto Kabwe ameahidi Kutatua changamoto ya ardhi inayowakabili wananchi wengi iwapo atachaguliwa. Soma Pia: GE2025 - Zitto azindua Kampeni Kigoma Mjini aahidi kupigania haki za kiraia
  4. GE2025 Zitto Kabwe: Wanamuogopa sana Luhaga Mpina, ndio maana wakamuweka vizingiti

    "Chama chetu mnamo Agosti 06, kiliteua mgombea Urais na Mgombea Mwenza ndugu Luhaga Mpina na Mama Farma Ferej lakini Kwa sababu wanamuogopa sana mgombea wetu wakaanza kuweka vizingiti kumzuia mgombea wetu" ‎ ‎Hayo yamesemwa leo Septemba 22, 2025 na Zitto Kabwe Kiongozi mstaafu wa ACT Wazalendo...
  5. GE2025 Zitto: Siendi kufanya uchawa ili nipendelewe, naenda kuwasemea ikibidi kufoka

    Mgombea ubunge wa Jimbo la Kigoma Mjini kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameahidi kutokuwa tayari kufanya vitendo vya kujipendekeza 'uchawa' bungeni ili apendelewe, badala yake ataendelea kupigania haki za wananchi wake kwa nguvu zote, ikibidi hata kwa kufoka. Amesema hayo Septemba...
  6. GE2025 Zitto Kabwe: Ili kuepuka mikopo ya ‘kausha damu’ nitaanzisha mfuko maalumu ambao nitauwekea Shilingi bilioni 1 watu watakopa bila riba

    Haya unayayasema Bw Zitto yakawe kweli pindi utakapo chaguliwa. Lakini hiyo bilioni 1 mpaka utafute misaada mhhh! mbona naona zoezi hili litaishia njiani? ========================== "Ili kuepuka mikopo ya ‘kausha damu’ lazima kuwe na mbadala, na mbadala huo ni kuanzisha mfuko maalumu ambao...
  7. GE2025 Mwananchi ampa ujumbe mzito Zitto "tukiwapa kura msibadilike kama wenzenu, muwe wazalendo"

    Bora huyu mwanamama kasema ukweli mtupu! Maana hawa wanasiasa mida hii wanajua kuzisaka kura kweli kwa njia ila wakizipata wanatokemea kabisa hadi miaka 5 ipite. ================ "sisi hatupendi wawe karibu yetu wanapokuja kuomba kura hata wanapokuwa huko tuwaone tunahitaji mkiwa huko mtuone sio...
  8. GE2025 Zitto Kabwe: Tutakomesha mikopo ya kausha damu

    Kausha damu inalea sana watu wengi mtaani, sasa Bw Zitto kusema utaiondoa naona ni kama ni uongo mtupu! ================ Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Mjini kupitia ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema atakomesha mikopo ya kausha damu jimboni humo pindi akichaguliwa.
  9. SI KWELI Zitto awashukia wanaharakati walioko ughaibuni

  10. GE2025 Zitto nyumba kwa nyumba kuzisaka kura za ubunge

    Katika kuzisaka kura za Ubunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, leo septemba 17, 2025 kiongozi mstaafu wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ametembela nyumba moja baada ya nyingine kuomba wananchi kura hizo katika Kata ya Kagera. Soma pia: Zitto ambwaga Nondo kura za maoni ubunge Kigoma Mjini...
  11. GE2025 Walioahidiwa Ubunge ndani ya ACT Wazalendo ni watu wawili tu, Zitto Kabwe, Ado Shaibu. Wengine wanatumika tu

    Kutoka vyanzo vya kuaminika kwa asilimia 99.99 ni kwamba Ndani ya ACT Wazalendo ni watu wawili tu walio ahidiwa kubewa ubunge au kupewa ubunge nao ni Zitto Kabwe na Ado Shaibu katibu mkuu wa ACT Wazalendo. Hawa wana baraka kutoka Ikulu kwa Mamana pia hata kwa Mgombea mwenza wa CCN Nduhmgu...
  12. GE2025 Rais Samia alivyokwepa kumrushia vijembe Zitto Kabwe kufuatia maneno ya Baba Levo

    Mgombea Urais kupitia CCM Samia Suluhu Hassan amesema kwa Jimbo la Kigoma Mjini Wagombea Ubunge wa mwaka huu wa CCM Clayton Revocatus Chipando maarufu kama Babalevo na Zitto Zubeir Kabwe wa Chama cha ACT Wazalendo wote ni wanae na wananchi ndio watakaoamua nani awaongoze. Dkt. Samia ameyasema...
  13. Kumbe Zitto Kabwe ni bonge la kupe

    Sitii neno. Naleta kama ilivyo. Najua Zitto Kabwa yumo humu. Huenda atatuelezea dhamira na nia yake ni nini. Je, namna hii hajawa bonge la kupe tena la kujipeleka? Je, imekuwaje akamuacha Mpina na kumpigia kampeni mama yake? Je, amelishwa kitu? Namna hii, ACT Wazenguaji itashindwa kuwa...
  14. GE2025 Zitto Kabwe: Othman anafaa urais Zanzibar anabebwa na rekodi zake

    Kiongozi mstaafu wa ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amesema mgombea urais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman kwa tiketi ya chama hicho ndiye anayefaa kuongoza kisiwa hicho kutokana na kuwa mstari wa mbele wa kupigania masilahi ya Wazanzibari. Zitto ameeleza hayo leo Jumamosi Septemba 13, 2025 wakati...
  15. GE2025 Zitto: Sasa kuna Uchaguzi, chaguo ni CCM iliyoshindwa kwa Miaka 60 au ACT ya mabadiliko

    Ameandika Zitto Zuberi Ruyagwa Kabwe "Sasa unaweza kusema kuna Uchaguzi. Wananchi watakuwa na chaguo la wazi kati ya CCM ile ile iliyoshindwa kuendesha nchi kwa miaka 60, gharama za maisha juu, huduma duni za Afya na watu 14M kudumbukia kwenye umasikini katika miaka 5 iliyopita ama ACTwazalendo...
  16. GE2025 Zitto Kabwe: Kazi inaanza kwenda kuzitafuta kura, baada ya Mahakama Kuu kuamuru Mpina ana haki ya kurejesha fomu ya urais

    Kiongozi Mstaafu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema mara baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma kuamuru kuwa Luhaga Mpina ana haki ya kurejesha fomu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, safari ya kusaka kura inaanza rasmi. Akizungumza leo Septemba 11...
  17. Watanzania mkataeni yule mstaafu wa ACT kutoka Magharibi anapokuja kuomba kura. Huyo ni mradi wa CCM

    Watanzania msikubali kurubuniwa na huyo anayetoka kanda ya magharibi mwa ziwa Tanganyika tambueni kuwa huyo siyo mpinzani bali ni mradi halali wa chama tawala( CCM). Wapinzani halisi ni chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ambao wanadai reform zifanyike ndio washiriki uchaguzi...
  18. GE2025 Shuhudia nyomi linalomsindikiza Zitto Kabwe kwenye mkutano wa kuzindua Kampeni za Uchaguzi Kigoma

    https://www.youtube.com/watch?v=vjOkard2ik0 Mwanasiasa mkongwe Zitto Z. Kabwe ameanza mchakato wa kampeni za kuwania Ubunge, leo Jumamosi tarehe 6 mwezi wa 9, 2025 anazindua kampeni Mkoani Kigoma.
  19. Zitto Kabwe anayesema Mpina atawafunga Mafisadi kama Magufuli,ndiye Zitto aliyetutukana kama tunampenda Magufuli basi tukazikwe nae Chato

    Chawa wa Mama aliyediliki kusema kama mnamoenda sana Magufuli basi nendeni mkazikwe nae,je yeye amezikwa na Mama yake aliyekuwa anampenda,hili lilikuwa tusi kubwa sana kwa Watanzania,baada ya hapo Hajawahi kumuongelea vibaya Mama Samia hata kidogo licha ya Ufisadi kukithiri zaidi ya awamu zote...
  20. M

    Watu wa Kigoma niwaelewa sidhani kama watachagua huyu comedian wa CCM na kumuacha Zitto Kabwe

    Yaani wapeleke bungeni commediana na chawa kama huyu Alafu waache msomi kama Zitto Haiwezekani japokuwa ana mapungufu.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…