Katika kapneni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025, baadhi ya wagombea ubunge wa Mkoa wa Dar es Salaam, wametoa ahadi wakigusa kero za wananchi.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), mwaka 2022 Dar es Salaam ilikuwa na wakazi milioni 5.4 na ni mkoa unaokua kwa kasi...