Aidha ripoti ya maendeleo ya binadamu ya mwaka 2013 iliyozinduliwa na Umoja wa Mataifa, ilibainisha zaidi ya nchi 40 zinazoendelea zilifanya vizuri zaidi ya matarajio katika maendeleo ya binadamu ndani ya miongo iliyopita karibuni, huku mafanikio yao yakiserereka pasina kushuka kasi na viwango...