Ni ngumu kufurahia mapenzi ikiwa una hofu au visasi vya kuumizwa

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
9,235
2,000
Ndugu zangu!

Tujilazimishe tu kusamehe na kuachilia. Sio kitu rahisi, lakini faida zake ni kwa maslahi ya kesho yako. Kwenye mapenzi unakutana na mtu ambaye humjui, unajifariji eti utamfahamu kupitia maelezo yake! Hii ni kujitekenya pakubwa.

Wengi wana yao mioyoni na hutoweza kuyajua, wenye majuto na hofu ya kuumizwa wapo. Wenye visasi vya kulipiza wapo, wale waliokata tamaa na kuona 'itakavyokuwa' tu nao ni wengi tu.

Kwa namna hizi na nyingine, iwe ni wewe au yeye. Ukiingia kwenye mahusiano mapya na kumbukizi mbovu au machale machale huwezi kufaidi mema walahi.

Tujifunze kusamehe na kujitakasa, waliokuumiza ni wengine sio huyu mwingine. Anza upya, na ufurahie maisha.

Ncha Kali.
 
Elli M

Verified Member
Mar 17, 2008
42,348
2,000
Tujifunze kusamehe na kujitakasa, waliokuumiza ni wengine sio huyu mwingine. Anza upya, na ufurahie maisha.
Barikiwa sana

IMG_20210619_195307.jpg
 
T14 Armata

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
4,057
2,000
Shanny baada ya kuachana na mpenzi wake aliye interim kwa sasa akanikubalia mimi. Nilikuwa namtafuta kwa mwaka hivi na attention yote nampa, wakati huo nina short term contracts na wadada wengine. Tatizo likaja pale nimeanza kuwa nae analeta kumbukumbu za ex wake.

Mara ya mwisho naonana nae alitoa kauli eti hawezi kunipenda kama alivyomoenda yeye. Akatoa sababu eti alimshauri huyo MD mambo mengi akafanikiwa alafu kamuacha yakiwa yameanza kutiki. Hebu niishie hapa kueleza
 
Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
10,472
2,000
Tiba sahihi ktk mapenzi ni kupata mtu wa kufanana (kuendana) naye kisawasawa.

Lkn hata ujitie kusahau vipi kama ukimpata mtibua nyongo lazima ukumbuke yaliyopita.

Sexless kungwi la kitaa
 
Will jr

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
2,401
2,000
Shanny baada ya kuachana na mpenzi wake aliye interim kwa sasa akanikubalia mimi. Nilikuwa namtafuta kwa mwaka hivi na attention yote nampa, wakati huo nina short term contracts na wadada wengine. Tatizo likaja pale nimeanza kuwa nae analeta kumbukumbu za ex wake.

Mara ya mwisho naonana nae alitoa kauli eti hawezi kunipenda kama alivyomoenda yeye. Akatoa sababu eti alimshauri huyo MD mambo mengi akafanikiwa alafu kamuacha yakiwa yameanza kutiki. Hebu niishie hapa kueleza
Usiwaze komaa naye atamsahau akikuzoea, hizo mbwembwe za short run
 
uungwana classic

JF-Expert Member
Jun 9, 2014
2,278
2,000
Ni kweli waliokuumiza ni wengine lakin jua kuwa hawatoki sayari nyingine ni hii hii na unatakiwa kujifunza kutokana na makosa machale muhimu sana hase siwezi umizwa kipuuzi mara ya kwanza na njia hiyo niumizwe mara ya pili, Ila sintakaa nihangaike kulipa kisasi kwenye mapenz et kisa nimeumizwa huko na mm nkaumize mtu baada yakugundu amenipenda
 
Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
9,235
2,000
Ni kweli waliokuumiza ni wengine lakin jua kuwa hawatoki sayari nyingine ni hii hii na unatakiwa kujifunza kutokana na makosa machale muhimu sana hase siwez umizwa kipuuzi mara ya kwanza na njia hiyo niumizwe mara ya pili, Ila sintakaa nihangaike kulipa kisasi kwenye mapenz et kisa nimeumizwa huko na mm nkaumize mtu baada yakugundu amenipenda

Huo sio uungwana classic!
 
Killboy

JF-Expert Member
Nov 2, 2019
1,080
2,000
Vidada vinavyosoma MD vinajiona kama dunia hii ni yao peke yao
Shanny baada ya kuachana na mpenzi wake aliye interim kwa sasa akanikubalia mimi. Nilikuwa namtafuta kwa mwaka hivi na attention yote nampa, wakati huo nina short term contracts na wadada wengine. Tatizo likaja pale nimeanza kuwa nae analeta kumbukumbu za ex wake.

Mara ya mwisho naonana nae alitoa kauli eti hawezi kunipenda kama alivyomoenda yeye. Akatoa sababu eti alimshauri huyo MD mambo mengi akafanikiwa alafu kamuacha yakiwa yameanza kutiki. Hebu niishie ha
 
kakamina

Senior Member
May 23, 2021
113
250
Ndugu zangu!

Tujilazimishe tu kusamehe na kuachilia. Sio kitu rahisi, lakini faida zake ni kwa maslahi ya kesho yako.

Kwenye mapenzi unakutana na mtu ambaye humjui, unajifariji eti utamfahamu kupitia maelezo yake! Hii ni kujitekenya pakubwa.

Wengi wana yao mioyoni na hutoweza kuyajua, wenye majuto na hofu ya kuumizwa wapo. Wenye visasi vya kulipiza wapo, wale waliokata tamaa na kuona 'itakavyokuwa' tu nao ni wengi tu.

Kwa namna hizi na nyingine, iwe ni wewe au yeye. Ukiingia kwenye mahusiano mapya na kumbukizi mbovu au machale machale huwezi kufaidi mema walahi.

Tujifunze kusamehe na kujitakasa, waliokuumiza ni wengine sio huyu mwingine. Anza upya, na ufurahie maisha.

Ncha Kali.
UKOKIKI (UKOSEFU WA KINGA KIMAPENZI), hili ndiyo tatizo kubwa Kwa watu wengi , watu walio na kinga za kutosha ktk mapenzi hawawezi kuwa Lia Lia Kwa kuwa kinga imara huwapa nguvu ya kuzuia mfadhaiko unaweza kupatikana kwenye relationship ya KIMAPENZI yeyote

Hawa ni watu ambao hawapati shida ukijifaragua kinywako anakuongezea na mwendo

Ukitaka kifurahia mapenzi uwe na kinga imara

Narudia Kwa wanaume; ukiwa na mwanamke hesabu ni wako unapokuwa naye Tu , ukiachana naye usihesabu . Fanya hivi haitakuja kutokea umejuta
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom