Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi amesema kuwa licha ya Tanzania kukubali mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, bado wapo watu na baadhi ya vyama vinavyotumia demokrasia hiyo kama kichaka cha kufanya vurugu na kuchochea uasi ndani ya Taifa...