Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi amesema kuwa, Rais Dk.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua rasmi Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP) chenye uwezo wa kuzalisha Megawati 2,115, tarehe 22 Agosti 2026, katika eneo la mradi lililopo Rufiji, Mkoa wa Pwani.