foleni

  1. Foleni Kimara Stop Over mpaka Suka - tarehe 16.08.2025

    Habari za jioni wakuu. Nimepita mida hii jioni leo tar 16.08.2025 mitaa hiyo ya Kimara Stop Over kuelekea Suka na kukuta kamba ndefu kiaina, lakini sababu leo ni gari dogo kuungua likiwa barabarani. Sijajua chanzo cha gari hilo aina ya Toyota Premio New Model kuwaka moto.
  2. Foleni kubwa Kiluvya Madukani na Mpiji

    Foleni ya kwenda kibaha imeanzia eneo linaitwa kwa Komba ni ndefu inaweza kufika urefu wa kilometa 2 au 3. Wahusika wasaidieni hawa wananchi waendelee na mishe mishe zao
  3. Foleni kali sana Ubungo - Kimara

    Aisee, hii kamba ya leo tarehe 13.08.2025 ni ndefu sio kitoto. Yaani kutoka Ubungo mpaka Kimara umbali wa kilometa 5 tunatumia masaa 2:30. Tatizo nini, ni ujenzi wa barabara au kuna ajali? @Tanroads
  4. Fredy Mwanjala: Madereva wasiofuata taratibu ndio sababu ya foleni Kituo cha SGR Morogoro

    Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetoa taarifa kuwa ajali ya treni ya Mjini kwenda Pugu, iliyotokea Stesheni ya KAMATA kwenye makutano ya reli na Barabara ya Kawawa, jana Mei 13, 2025 imejeruhi Watu 10 TRC imesema ajali hiyo iliyohusisha mabehewa 12 yaliyobeba abiria takribani 1,200 na kuwa...
  5. Serikali yaja na suluhisho la foleni mpaka wa Tunduma

    Serikali mkoani Songwe imesema kuwa suluhisho la kudumu la changamoto ya foleni katika mpaka wa Tunduma ni ujenzi wa bandari kavu katika eneo la Mpemba, pamoja na ujenzi wa barabara yenye njia nne, ambao tayari umeanza katika upande wa Mkoa wa Mbeya kuelekea Tunduma. Pia soma ~ Foleni ya...
  6. A

    KERO Barabara ya kuelekea Msumi ni mbovu sana kupelekea foleni kila kukicha

    Ni kero ya muda mrefu na inaendelea kutuumiza wakazi wa makabe kuelekea Msumi. Porojo za siasa zimekuwa nyingi huku wananchi wanateseka huku wahusika wakikaa kimya . Muda huu kuna foleni kubwa sana na njia mbovu . Mkuu wa wilaya ya Ubungo ahadi zako hazitimizi huku wananchi wanateseka
  7. Katikati ya mji wa Arusha, kuna foleni sana, mji ni mdogo

    Ukiwa katikati ya mji wa Arusha, maeneo ya stendi kuu, soko kuu, jogoo house, kilombero na maeneo mengine kuna foleni sana. Foleni ya mabasi makubwa, coaster, bajaj, bodaboda hadi foleni ya watembea kwa miguu. Mji umekuwa ni mdogo sana, Geneva ya Afrika mnakwama wapi?
  8. W

    Msafara wa ndege za kivita za Marekani waelekea Mashariki ya kati baada ya Trump kutoa agizo la dharura raia wa Iran kuondoka Tehran, foleni imeshona

    Baada ya agizo la Dharura, Foleni ya kuondoka Tehran imekuwa ni kubwa sana, Trump kalazimika kukatisha mkutano unaoendelea nchini Canada wa G7 na kurudi haraka Marekani, Amewaagiza wajumbe wa Baraza la Usalama wa Taifa (NSC) wawe tayari kwenye chumba cha dharura (Situation Room)...
  9. Maoni yangu kuhusu Suluhisho la Msongamano wa Magari Jijini Dar es Salaam

    Nimeona jitihada zinazofanywa na wadau katika siku za hivi karibuni kutafuta suluhisho la tatizo sugu la msongamano wa magari jijini Dar es Salaam, ikiwemo hatua ya kufunga kamera za ufuatiliaji barabarani. Hata hivyo, kwa mtazamo wangu, matumizi ya kamera hayawezi kuondoa tatizo la foleni kwa...
  10. KERO Responded Foleni ya Tunduma mpakani haitatuliwi, kuna Watu wana maslahi Binafsi, inatutesa wengi

    Wazee huku Tunduma ni changamoto kuvuka aisee siku saba foleni haitembei, huu msongamano wa malori katika mpaka wa Tanzania na Zambia upande wa Tunduma ni kero kubwa sana na hali hii inakwamisha Uchumi wa watu wengi na unawafaidisha wachache. Kuna kiongozi wa masuala ya Usalama (jina...
  11. Foleni chanzo Cha msongo wa mawazo katika barabara za Jiji la Dar Es Salaam

    Imeelezwa kuwa tatizo sugu la foleni katika barabara za jiji la Dar es Salaam linaweza kuongeza msongo wa mawazo kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri, kuchochea uchovu kwa madereva na abiria na hatimaye kuongeza uwezekano wa ajali na vifo barabarani. Hayo yamebainika katika wiki ambayo jiji...
  12. Changamoto ya Foleni njia ya Moshi-Arusha

    Barabara ya Moshi-Arusha magari hayatembei kuanzia Kia mpaka Arusha Mjini. Haijulikani changamoto ni nin hasa na wale wa kutoka moshi kwenda arusha wametanua njia nzima na wale wa kutoka arusha kwenda moshi nao wamefanya hivyo hivyo. Wahusika wenye mamlaka watatue changamoto hii kwani ni zaid...
  13. Dar: Sam Nujoma Road leo kuna foleni hata kuelezea haiwezekani!

    Huu mji mgumu aisee. Ikifika hii mida ya kurudi majumbani kuna foleni aisee gari hazitembei kabisa. Kama jioni hii una rwtiba ya kutumia hii barabara fikiria mara mbili.
  14. Foleni kubwa Kunduchi Mbuyuni leo nzima

    Kutokana na lori la mafuta lililoanguka Kunduchi limezua foleni kubwa siku nzima ya leo Tunaomba wahusika walitoe tupumue Maana wameanza kunyonya mafuta
  15. T

    Foleni ya Kibaha Chalinze itaisha lini?

    Huwa nasikia awamu hii imefanya mambo makubwa. Kuna hii barabara inayounganisha bandari ya Dar na mikoa karibu yote nchini, lkn pia nchi jirani zinazotumia bandari yetu. Cha ajabu ni kwamba barabara ya Kibaha Chalinze bado ni nyembamba sana hivyo kusababisha foleni kila siku. Sasa hivi...
  16. Itakuwa tukio la kukumbukwa pale ma-captain wa vivuko vya Kigongo Busisi watakapopanga foleni kuwaaga wananchi waliowahudumia kwa miaka zaidi ya 50

    Moja kati ya matukio muhimu ambalo nataraji litapewa nafasi, ni kwa hawa manahodha wa vivuko kuandaa kama ki-parade hivi, wakiwa na mavazi yao meupe, kofia zao, huku wakipunga bendera ya taifa kuashiria kwamba wamekamilisha kazi yao ya kishujaa kwa uaminifu na uzalendo mkubwa, na sasa wanawaaga...
  17. Foleni kali kuanzia Goba centre mpaka njia nne kueleka mbezi mwisho, ni janga lingine linalokua kwa kasi

    Habari wakuu, Siku za hivi karibuni kumekua na foleni kali sana kuanzia saa kumi na mbili jioni kuendelea, foleni hiyo inaanzia pale Goba centre mpaka njia nne na ile barabara ya kuelekea mbezi mwisho, mara kadhaa nimeshakutana na hii foleni nyakati za jioni nikiwa natoka kazini, imekua kero...
  18. W

    Wananchi wengi wa Denmark huendesha baiskeli ili kuepuka foleni na msongamano kwenye mabasi. Watu 9 kati ya 10 wanamiliki baiskeli nchini humo

    Watu wengi nchini Denmark, hasa wanaoishi mijini, wanapenda sana baiskeli zao. Hufanya hivi ili kupata uhuru binafsi ambao unawapa fursa ya kuingia na kutoka kwenye msongamano wa magari mjini. Ukiwa kwenye baiskeli, huhitaji kusubiri kwa muda mrefu. Huhitaji pia kungoja basi lifike au kuingia...
  19. Kumekuwa na ongezeko la foleni kubwa jijini Dar es Salaam hivi sasa!

    Kumekuwa na ongezeko la foleni kubwa jijini Dar es Salaam, hasa kwenye barabara za kutoka Mwenge kwenda Tegeta, Mwenge kwenda Buguruni, na Posta kuelekea Mwenge, hasa nyakati za asubuhi na jioni. Je, sababu ni magari kuongezeka? Au ni miundombinu ya barabara kuwa mibovu? Au ni kutokana na...
  20. Video: Foleni ya Kimara - Ubungo ni balaa mchana huu kuelekea Mbezi

    Wakuu Foleni katika barabara ya Morogoro kipande cha Kimara hadi Ubungo kutokana na ujenzi unaendelea.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…