Hapo umepigwa ama unatupiga, haiwezekani atoke banana aje palestina huu ni uongo, yaani kapanda magari mawili mpaka matatu kufika palestina,
Hiyo karatasi ya dawa anatembea nayo akiona mtu anayeeleweka tu anaomba msaada hata mwananyamala kuna kijana ndo kazi yake
Wodi ya wanawake namba nne gorofa ya kwanza mwaisela muhimbili huduma ni za kuomba, mgonjwa anahitaji huduma kama kipimo inabidi asubiri mpaka ratiba ya kipimo hicho ifike mgonjwa anaumwa kweli unasubiri siku ya hicho kipimo, wagonjwa wanang'atwa na mbu balaa, ukilazwa unapata na maralia...
Nilichoelewa ni unatakiwa uwe bahili, usiwe mtu wa tamaa kwa kila unachoona kwakuwa una hela basi unanunua tu hata kazi ya hicho kitu huna, ama ni ile kwenda na matoleo kila toleo unataka, huweki akiba hata kidogo ukipata shida tu kidogo lazima ukakope kausha damu mara wezesha mara ile voda...
Nenda branch omba wakupe card kwa sasa zinatolewa baada ya malalamiko mengi ya mawakala network, kabla mteja hajaondoka angalia statment na mteja wa luku usirudishe hela asubiri token atatumiwa
Ninavyojua hela ukikosea namba ikaenda kwa wakala hapo hapo ukipiga cm inazuiwa wao watampigia cm wakala ataulizwa kama amekuhudumia akisema sijamuhudumia hapo hapo ama kesho hela inarudi, labda ulikosea namba ya mteja akawa katoa
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.