Kuna jirani yangu pia alikuwa anasumbuliwa sana masuala ya kodi na mpangaji wake, yule mpangaji akawa anataka apewe notisi ya miezi 3 akae bure akidai ndiyo sheria inavyosema.
Ikabidi mwenye nyumba aende serikali ya mtaa kumshitaki, hukumu iliyotoka mwenyekiti wa serikali ya mtaa alimwambia...
Mkuu upo sahihi kabisa, nipo nchini Singapore [emoji1215] hapa sasa hivi wahindi wamejazana kila kona, bandarini stevedores wote ni wahindi, vibarua vya ujenzi, usafi ni wao tu.
Sijamuona mwafrika ni wao tu ndiyo wanatamba, ila uzuri wao wengine wasomi wanafanya kazi nzuri tu.
Ni kweli kabisa mkuu unachoandika, Bakhressa lengo lake kubwa ktk kuanzisha UFM ni kutangaza biashara zake. Na ndiyo maana huwezi kusikia UFM ikitangaza matangazo ya kamari kama wanavyofanya hao Wasafi media au Clouds media.
Mkuu kabla mzigo haujaisha usiache kutuambia kule wanakotengeneza madawa Fatemeh alipokuwa anaonesha dalili za arosto alikuwa anakimbilia kwenye kibanda kujitibu vipi na arosto.
Kama pesa unayo poa tu siyo mbaya kumpeleka mtoto shule za gharama, shida inakuja kuna watu uwezo hawana halafu wanalazimisha kuwapeleka shule za ghali matokeo yake wanaanza kuwasumbua ndugu na jamaa kwa kuwaomba waongezewe pesa ya ada ya mtoto wake anayemsomesha shule za ghali.
Mkuu huu mchongo uliompatia itakuwa bora zaidi aende chuo cha bahari Dar Es Salaam Maritime Institute(DMI) kusoma kozi za kibaharia (mandatory course).
Huwezi kufanya kazi ya upishi melini kama hauna vyeti hivyo (First Aid, Fire [emoji91] Fighting, Personal Survival Techniques, Personal Safety...
Hata Kigogo Mburahati au Luhanga au Mabibo kwa hela hiyo unapata nyumba nzuri ya kupanga. Usafiri ni mwingi hauna shida maeneo hayo.
Hata siku ukiamua kwenda Posta kwa miguu unaweza, ni mwendo wa lisaa limoja tu kwa mwendo wa kijana usiokuwa wa kiuvivu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.