Maongezi vijana wa Tanzania; 96% ni pumba

Maongezi vijana wa Tanzania; 96% ni pumba

Kweli ni wachache sana kama wapo utakao kuta wananunua magazeti kama Mwananchi, Mwanahalisi, Mseto, Nipashe au Mtanzania. Lakini yale ya udaku mara sikui wema kalala na diamond, mara mtu kafumaniwa, mara zari na wema moto juu nk ndio magazeti yao tena hasa wasichana. Kwenye redio wao sana sana ni zile za miziki na tv huwezi kukuta wanaangalia BBC, Aljazeera, ITV au TBC sana sana ni chan 5 na clouds
mimi ningekuwa kiongozi hayo magazeti ya udaku yote ningeyafungia ...nimeshajito kwenye magroup yote ya watsaap ambayo ni ya kipuuzi "" kubwa zaidi nilipokuja kujua kuwa jf nijukwaa pana linaloweza kuelimisha ndio nimejikuta hata radio na TV sifuatilii ...instagram yenywe nime I unstore kwaajili ya huo upuuziwa wema na na zari alikiba na diamond...sikatai Nina group LA michezo but lipo kwaajili ya kujifurahisha kwa sabbu michezo nikiburudisho na huwa naingia Mara chache mnoo maana hta text nimezi mute....tukubali tukatae vijana twajitaji mabadiliko makubwa mnoo yakifikira...unapojigundua kuwa unajitambua then ukaanza kupiga msasa wakupunguza watu wasiojielewa waweza jikuta umebakia na marafiki. wawili tu
 
Tuacheni tunajadili yanayofurahisha nafsi zetu
kama unaona unakereka tafuta mahali ukaishi
hapa mpira tu mpaka mpira uachwe kuchezwa
hhaaaahaa aiseee hebu ficha huo unazi wako basii
 
Sasa kama unatumia siku nzima kumpigia kura unaemtaka lkn kura yako akapewa usiyempigia kwa nguvu ya mtutu wa bunduki, kwa nini nisimjadili King Messi na Ronaldo? Mnataka tujadili takwimu za Uchumi zilizopikwa na Serikali yanu haliyakuwa mmetupiga bann?!
 
Vijana wengi wa kitanzania (Sehemu za miji mikubwa ikiwemo Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya) 96% ya maongezi yao ni pumba tupu na vitu visivyowasadia katika kujikwamua kimaisha ikiwemo mpira wa ulaya (FA, EPL, UEFA n.k.), Wasanii wa bongo na skendo zao, namna mheshimiwa anavotumbua majipu. Ni ngumu kumkuta kijana wa miaka 18 - 35 akiongea vitu vya maana vya kujenga uchumi (binafsi, jamii na taifa) kwa muda unaozidi dakika 5 mfululizo bila kuchomeka Tusi.

Hivi interview/kazi huwa mnapataje aisee? na bomba la mafuta tumeambiwa linapita Tanzania kweli namna hii mtapata kazi kweli? au ndo watajaa wa kenya kama kawaida?

NB: Fuatilia kwa wauza magazeti, vijana wengi hununua magazeti ya michezo, udaku n.k. na kuacha magazeti yenye fursa na habari za maana kwa mustakabali wa nchi. Sad!
Ni kweli mkuu ...yani pumba nyingi mpira na udaku ndo habari kuu....ndo mana mm hata siku moja huezi kunikuta eti nimekaa na wadau tunapiga stori bora nilale ndani au nikae na dem wangu
 
Watu kuzungumzia uchumi nk.. haimaanishi kwamba ndio watakuwana maisha mazuri..

Tatizo serikali imeeka VIPAUMBELE wapi na kweny nn ili uchumi wa nchi Ukue na kuongeza wigo mpana wa Ajira kwa hilo kundi kubwa la 98% ambalo unasema linaongea upuuzi tuu..

Kama serikali ime invest kweny Fitna, Chuki,Roho mbaya, na siasa chafu na kupikapika data na kusifiasifia Ujinga na kujipendekza ili mtu aonekane kafanya kitu..Sahau maendeleo.

We are in the SHITHOLE country even ideas nazo ztakuwa ivo ivo...
Acha tuendelee kucheza TATUMZUKA ipo siku tutatusua.
 
Vijana wengi wa kitanzania (Sehemu za miji mikubwa ikiwemo Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya) 96% ya maongezi yao ni pumba tupu na vitu visivyowasadia katika kujikwamua kimaisha ikiwemo mpira wa ulaya (FA, EPL, UEFA n.k.), Wasanii wa bongo na skendo zao, namna mheshimiwa anavotumbua majipu. Ni ngumu kumkuta kijana wa miaka 18 - 35 akiongea vitu vya maana vya kujenga uchumi (binafsi, jamii na taifa) kwa muda unaozidi dakika 5 mfululizo bila kuchomeka Tusi.

Hivi interview/kazi huwa mnapataje aisee? na bomba la mafuta tumeambiwa linapita Tanzania kweli namna hii mtapata kazi kweli? au ndo watajaa wa kenya kama kawaida?

NB: Fuatilia kwa wauza magazeti, vijana wengi hununua magazeti ya michezo, udaku n.k. na kuacha magazeti yenye fursa na habari za maana kwa mustakabali wa nchi. Sad!
Ukitaka mali utaipata shambani, iweje leo upate mali kijiweni bila kufanya kazi? warudi vijijini wakalime mbona si tuko huku bush tunaenjoy tu.
 
Kwa masikitiko makubwa hao vijana wa kwenda kushika jembe hawapo tena. Mtu kazoea kusuguliwa ndo apate pesa jembe ataliwezea wapi?
 
dunia nayo inawahitaji waongea pumba na wapumbavu ili waelevu waonekane..uelevu wao dhidi ya wapumbau na waongea pumba...
 
Kwenye magroup ya Whatsapp kumejaa pumba tupu. Yesu njoo mapema uchukue watu wako maana wanaangamia kwa kukosa maarifa.
[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Yani umegonga penyewe Mkuu huu ni ukweli kabisa.
Mimi ni kijana na nakubali hayo usemayo japo sijajua kama ni utafiti huo au laa
 
Ukiwa Kenya, panda matatu (kwetu daladala) vijana wengi wanazungumza jinsi ya kujikwamua kiuchumi. Mara usikie niliopokuwa Nairobi University professor fulani alinifundisha namna ya kuandika project (kubuni mradi kwa mpangilio). Utasikia hivi ardhi nzuri kwa vitunguu saumu ni ipi? Na mambo mengi ya maendeleo. Hapa bongo ni mambo ya michezo ya Ulaya na mambo ya udaku wanaagana, jioni tukutane bar fulani. Kwa hali hiyo taifa litajengwaje? Halafu huko Kenya ni lugha iliyonyooka ya kiingereza na kwetu ni kiswahili kilichopinda. Ni wakati wa kuamka tena tukimbie badala ya kutembea
Naomba vitu muhimu wakati wa kuandika project tafadhali.
 
Back
Top Bottom