Mbunge wa Tarime John Heche kupeleka hoja binafsi muda wa Urais, Ubunge upunguzwe

Mbunge wa Tarime John Heche kupeleka hoja binafsi muda wa Urais, Ubunge upunguzwe

Mbona mmeshindwa kutoa hoja binafsi Chamani kwenu ya kwamba muda wa Mwenyekiti/Mmiliki wa Chadema Taifa upunguzwe!? [HASHTAG]#ChademaMnazingua[/HASHTAG].
Cc: Petro E. Mselewa.
 
tatizo letu kwenye mambo yenye faida kwa Taifa tunaingiza huko mambo ya vyama vya siasa huo ndo upuuzi unafanyika Tanzania wabunge wengi wa chama tawala wapo kwa maslahi yao binafsi kuliko maslahi ya Taifa. Mbunge John Heche ameonyesha njia tunategemea wabunge wote kumuunga mkono katika hoja yake.
Angeonyesha njia ya mabadiliko ya Mwenyekiti/Mmiliki wa Chadema kwanza. Acheni UZANDIKI nyinyi na kuchezea akili na fikra za Watanzania.
 
Mbunge wangu nakuunga mkono.ila uangalie usiitwe mchochezi.
 
Wabunge wa ukawa wapo wangapi bungeni TENA wabunge hao wana njaa, eti wakubali kupunguza muda! Unajua salio lao la mwaka wewe mpaka wakubali?? Heche mwenyewe hawezi kubali, ni kwamba kaamua tu kuchezeshwa singeli la Nkamia!
Uwe unafikiri kabla ya kuandika
 
Iwe miaka miwili miwili tu... Daaah ungekuta Baba Jessica na mwanae bashite wamebakiza mwaka tu.
 
Wabunge wa ukawa wapo wangapi bungeni TENA wabunge hao wana njaa, eti wakubali kupunguza muda! Unajua salio lao la mwaka wewe mpaka wakubali?? Heche mwenyewe hawezi kubali, ni kwamba kaamua tu kuchezeshwa singeli la Nkamia!


Muhimu ni uzito wa hoja yake. Swala.la.kupita au la ni la upimbavu wa wapitishaji na tafsiri ya aina gani ya watu tulivyo.
 
Naunga mkono hoja, I wish ingekuwa hata miwili leo Magufuli angekuwa amebakiza miezi miwili ingekuwa furaha iliyoje kwa Watanzania.
Kwa Rais anatakiwa awe under brobation ya nusu mwaka akifail kama dikteta anatimuliwa
 
Wote tu wanatafuta kiki tu mbona suala ya Posho kupungua hawataki kwa pamoja si utawala wala upinzani.

Marekani si kila jambo tuwaige tuwe kama South Africa ama Brazil au South korea kuwa na bunge lenye kumuondoa Rais madarakani
 
Nakubaliana naye kwani mtu huhitaji mamiaka mengi madarakani kama kweli unachapa kazi.

Hata miaka mitatu inatosha kabisa kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo.
Lkn NN wafariji ndivyo tulivyo nakubaliana na ww.
Hapa huyu Heche unamjibu nkamia anayetaka iwe miaka 7. Nkamia yy anataka kuchukua tumbo hilo tunalijua
 
Mbunge wa Tarime Vijijini kupitia (CHADEMA) John Heche amefunguka na kusema anakusudia kuwasilisha bungeni hoja binafsi ili kupunguza muda wa viongozi kukaa madarakani kutoka miaka mitano na iwe miaka minnee kama Marekani.

John Heche amesema hayo leo kupitia mitandao yake ya kijamii zikiwa zimepita siku kadhaa toka Mbunge wa Chemba Mhe. Juma Nkamia (CCM) kusema anatarajiwa kuwasilisha muswada binafsi bungeni kulitaka bunge kufanya marekebisho ya katiba ili viongozi waweze kukaa miaka saba. Jambo ambalo Heche anapinga na kusema kuwa muda ambao viongozi wanakaa madarakani ni mkubwa sana.

"Nakusudia kuwasilisha bungeni hoja binafsi kupunguza muda wa kukaa madarakani kwa Rais, wabunge na madiwani kutoka miaka 5 mpaka 4 tuwe kama Marekani ili kutoa nafasi kwa wananchi kuwa na maamuzi zaidi kuhusu uendeshaji wa nchi yao" Alisema John Heche.

Aidha John Heche amesema kuwa kiongozi akikaa madarakani muda mrefu anajisahau na kuona ile nafasi kama ni yake pekee yake jambo ambalo si sawa hata kidogo
"ukikaa sana madarakani unafikiri nchi ni mali yako, kuna viongozi wengi sana wazuri ila hawajapata muda tu wa kuongoza" alisisitiza John Heche.
View attachment 591072

This is now kidding! One wants tenure extended to seven year, the other wants it shortened to four years. Political leaders are put in power by common citizens through a ballot box- and what is most important to voters is service deliverance at the first place. Extension of tenure will only be meaningful if is associated with services to common citizen, equally shortening of the period will equally make sense if and if only is associated with services to citizens
 
Si apatikane mwingine apeleke wake hata week mbili... hakuna kipindi kitamu kama cha kampeni kwani ccm uwa wanawachangamsha sana mama zetu mara usiku mama mwajuma kaja kuleta chumvi, skafu, kanga na flana za yanga... huku chadema wakitupa madini adimu na kutuonyesha wapi acacia walitupiga zile za tegeta zilichotwa vip... kipindi hiki hata wenye akili timamu huziweka mfukoni ili wapate huruma hata wa wasio waelewa ndo utakaposhangaa mbabu mzima akihangaika kutafuta six pack hata kwa kupiga push up jukwaani ili watu waamini ni mzima wa afya kumbe wajuzi wa mambo wakitaka watu wazima wa akilini... hahaha kipindi hiki uwa kizuri sana nchini mwetu... mtaani kwetu igoma uwa hatulali hasa siku ya matokeo dah fanyeni wiki mbili bas wadau
 
Hoja ujibiwa kwa hoja tena sehemu sahihi na katika muda sahihi. Safi sana mbunge wewe japo ckujui
 
..YES.

..lakini miaka 7 anayopendekeza Mh.Nkamia ni mingi mno.

..mimi napendelea miaka 5 au 4. Isizidi au kupungua.

..naamini kipindi hicho kinatosha kwa waliochaguliwa kusimamia na kutekeleza waliyoahidi.

..vilevile naamini kipindi hicho kinatosha kwa wananchi kuona kama wanapaswa kubaki na, kubadilisha viongozi waliopo madarakani.

Nakubaliana na wewe, miaka 7 ni mingi. Tubaki kwenye 5 na kazi kubwa iwe kujenga mifumo imara ya public service.
 
hiyo ndio hoja ya kuunga mkono ili watu wengi wanauwezo wa kuongoza ili kila mmoja apate nafasi ya kutoa mchango wake
 
Back
Top Bottom