Mabadiliko kwenye mfumo wa chaguzi zetu hayapuuziki wala hayazuiliki. Pamoja na jeuri ya kichama na kidola, mabadiliko ni muhimu kama chumvi na ndimu kwenye supu adimu. Muhimu kama elimu ya kumkomboa mwanadamu kutoka zamadamu.
No Reforms, No Election imepata uungwaji mkono na sinema za CCM. Ni...
Najua hamtaniamini. Najua mpo mtakaobisha vya kutosha na kutisha. Mtapaniki kuliko pikipiki ya kutumia kiki. Lakini, nawaambia jambo hili. Ni jambo geni na kubwa lakini muhimu na linalowezekana kwenye siasa za sasa. Siasa za sasa zinahitaji amshaamsha.
Haifichiki tena kuwa mambo ndani ya CCM...
Nimeshindwa kuvumilia kutofuatilia na kushiriki siasa. Tangu miaka ya 80 nilipojiunga CCM baada ya kuhitimu masomo yangu pale Mlimani, nimejionea mengi. Nimewaona na kufanya kazi na wanasiasa waongo, wakweli, halisi na bandia. Wengi bado wapo, achilia mbali wale waliotangulia mbele ya haki...
Mwaka 2010, Tundu Lissu aligombea kwa mara ya kwanza nafasi ya ubunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya CHADEMA akiwa na umri wa miaka 42. Mgombea wa Urais wa CHADEMA alikuwa Dr. Wilbrod Slaa na huku wa CCM akiwa ni Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.
Kwa kauli yake mwenyewe, tena akiwa anatetea urais...
Haya ndiyo mambo ya kutumbuliwa ili kutambuliwa. Mawaziri wa zamani Nape Nnauye na January Makamba wamejumuishwa kwenye Kikosi Maalum cha CCM kinachoandaa Ilani ya CCM ya mwaka 2025 hadi 2030. Kikosi hicho kinaongozwa na komredi Stephen Wassira.
Nyaraka za kichama zinaonesha kuwa Nape na...
Tume hii ni Idara huru ya kiserikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa Katiba (rejea Ibara ya 129 (1)). Ina wajibu wa kuhakikisha, pamoja na mambo mengine, haki za binaadamu na utawala bora vinatamalaki. Tume hii hupokea malalamiko; huyachunguza na kutoa ripoti zake.
Katika siku za hivi karibuni...
Ingekuwa kwenye nchi ya kidemokrasia na inayoiishi demokrasia, Waziri Nape Nnauye angeshapoteza uwaziri na ubunge wake muda huu. Angepoteza kwa shinikizo la wananchi au kuondolewa na Rais aliyemteuwa. Lakini hapa kwetu, Nape bado anadunda na anakejeli kwa kusema eti amechakachuliwa video yake ya...
Suala la Mpina halipuuziki. Sema nasi tusikie. Mbunge Luhaga J. Mpina alidai bungeni kuwa Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amelidanganya Bunge kuhusu sakata la uingizwaji wa sukari nchini. Alidai, pamoja na mambo mangine kuwa Bashe alisema uongo zaidi ya mara kumi.
Kwa mujibu wa Mpina, Waziri...
Kichama na kiserikali namfahamu Komredi Kinana tangu miaka ya 80. Naujua uhodari wake kijeshi (kwakuwa nami nilitumikia mojawapo ya vyombo vya ulinzi na usalama), kiserikali na kichama. Komredi Kinana si mtu wa maneno mengi. Ni mtu wa mipango ya viwango na vitendo na mwendo.
Sikushangaa pale...
Unakaribia mwezi mmoja sasa tangu msafara Ndugu Paul Makonda, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, upate ajali kule Sululu, Masasi mkoani Mtwara. Ajali hiyo iliyohusisha magari yapatayo 10, ilitokea tarehe 11 mwezi uliopita na kusababisha uharibifu wa magari kadhaa yakiwamo ya...
Nipo hapa Arusha. Jana nami niliyashuhudia (lakini sikushiriki) maandamano ya amani ya CHADEMA katika viunga vya jiji la Arusha. Sikwami wala kuogopa kusema kuwa yalikuwa ni maandamano makubwa; washiriki walikuwa wamejipanga kila anga na yalipeperusha hoja za haja.
Kabla ya jana, nilioneshwa...
Sasa ni dhahiri kuwa suala la umeme linakitweza na kukiaibisha chama tawala-CCM. Pia, umeme unaitweza na kuiaibisha Serikali iliyopo madarakani. Umeme unakatikakatika. Umeme haueleweki. Umeme hauaminiki. Umeme hauzoeleki. Umeme unagawiwa. Unaleta athari kubwa kwa wananchi na kwa nchi.
Mimi...
Jana nilikusikia na kukusikitikia sana. Jinsi unavyojikaanga kwa mafuta yako mwenyewe. Jinsi unavyoonesha kuchoka na kukinai nafasi uliyonayo kwasasa chamani. Pale ulipozungumzia kuhusu mdahalo na viongozi wa CHADEMA.
Ngoja nikusaidie kwakuwa nilikuwa kiongozi mwandamizi chamani kabla yako...
Kwanza, tunamshukuru Mungu kwa kuzuia hujuma zisizo na huruma kwa CCM yetu baada ya kuepusha kupokwa kwa nafasi ya Katibu Mkuu jana. Shukrani zetu, kama makada waandamizi na wazee wa chama, ni kwa Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa Mama Samia S. Hassan kwa kutusikiliza tulipomshauri cha kufanya...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.