Recent content by T Kaiza-Boshe

  1. T Kaiza-Boshe

    JamiiForums Tanzania Mwanamke huyu asaidiwe, Mahakama imtendee haki

    Wote tunakubaliana kuwa ujangili ni mbaya, na ni kosa la jinai; na kwamba sawa kuadhibiwa kisheria! Na tunazo sheria za Uhifadhi wa Wanyamapori zinazotumika kulinda Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 na sheria Na. 383 kama zilivyorekebishwa 2023 zinazotuhusu watu wote; wananchi, na wageni pia...
  2. T Kaiza-Boshe

    JamiiForums Tanzania Kitabu cha Safari ya Ushindi ya Mama na Mtoto Mwenye Usonji (AUTISM)

    Video ya watoto wanaojibu swali kuhusu makabila yao haihusiani na post yangu kuhusu kitabu cha mama na mtoto mwenye usonji. Video imepop-up wakati nataka kuweka link ya mtoto mwenye usonji na ambaye ni genius wa ajabu; ana IQ kuliko Albert Einstein! Hiyo sikuweza kui-post. Nitajaribu baadae.
  3. T Kaiza-Boshe

    JamiiForums Tanzania Kitabu cha Safari ya Ushindi ya Mama na Mtoto Mwenye Usonji (AUTISM)

    Je, umesoma kitabu hiki? Angalia picha ya gamba (cover) lake kitabu hicho. Na, je, unajua maana ya usonji? Kwanza tuujue usonji (Kiingereza, autism) Usonji ni hali ya kuwa na changamoto za akili zinazoathiri uwezo wa mtu kuwasiliana na kuchangamana na wengine, pamoja na kuwa na tabia ya...
  4. T Kaiza-Boshe

    JamiiForums Tanzania JIHADHARI NA WIZI WA AJABU MPYA WA SIMU, HASA SIMU JANJA (CELLPHONE)

    Wengine wanauita utapeli, kwa maana simu utaitoa wewe mwenyewe, na inandoka ukiiona. Iko hivi, anakuja mtu unayemjua vizuri, na wakati mwingine humjui, anakuomba simu unampa; na anaweza kuchukua na ya mwingine, na ya mwingine. Nyote mtampa simu zenu! Manaweza kuuliza kwa nini, au ya nini, huyo...
  5. T Kaiza-Boshe

    JamiiForums Tanzania Tatizo la Usikivu Hafifu Tanzania

    Usikivu hafifu ni tatizo kubwa na linalokua Tanzania; lakini linaweza kupungua kama mamlaka husika zikitimiza wajibu wao kisheria kwa dhati. Naanza na mfano mdogo wa kuonesha ukubwa wa tatizo. Kwa mujibu wa Mwongozo wa Kitaifa wa Udhibiti wa Kelele na Mitetemo wa 2022, utafiti wa 2019 wa Chuo...
  6. T Kaiza-Boshe

    JamiiForums Tanzania Makelele ya makanisa kwenye makazi siyo sawa kidini, wala kisheria; yadhibitiwe kama makelele mengine

    Wakiswali kama wanavyoswali kiada, yaani dakika hizo chache za Azana, kujitayarisha, na kusali kwa muda usiozidi dakika ishirini, hawajavunja sheria. Kiafya nako siyo tatizo sana ndiyo maana swala hizo na misikiti imeendelea kuwepo kwenye makazi sehemu nyingi duniani. Ila, inasemekana, kuna...
  7. T Kaiza-Boshe

    JamiiForums Tanzania Makelele ya makanisa kwenye makazi siyo sawa kidini, wala kisheria; yadhibitiwe kama makelele mengine

    Naomba ifahamike kuwa si lengo la makala kulalamikia makanisa kwa misingi ya tofauti za kidini, bali kuzungumzia tatizo ambalo linahusu baadhi ya makanisa, na wala siyo yote. Ninazungumzia tatizo, na siyo makanisa, wala imani. Makanisa nayataja kwa uhusika wake na tatizo ninalozungumzia...
  8. T Kaiza-Boshe

    JamiiForums Tanzania Makelele ya makanisa kwenye makazi siyo sawa kidini, wala kisheria; yadhibitiwe kama makelele mengine

    Ahsante! Mtu yeyote, ama taasisi yoyote, anaweza kutenda kosa kwa kutojua, ila akijua hana budi kujirekebisha. Ila inapotokea mtu akatenda kosa akiwa anajua, ama akakaidi sheria, na asijali madhila ya kosa lake kwa wengine, inakuwa kosa kubwa sana kwa dini yoyote na jamii yoyote ile; na Mwenyezi...
  9. T Kaiza-Boshe

    JamiiForums Tanzania Makelele ya makanisa kwenye makazi siyo sawa kidini, wala kisheria; yadhibitiwe kama makelele mengine

    Ahsante kwa mchango wa mawazo. Katika makala hii wametajwa Wakristo kwa sababu tatu: 1) Mimi ni Mkristo, hivyo nafahamu miongozo ya Kikristo; ya Kiislamu siijui. 2) Sehemu kadhaa nilikokaa nyumba za ibada zinazopiga makelele yanayozidi viwango kisheria ni za Kikristo, hasa makanisa ya Kilokole...
  10. T Kaiza-Boshe

    JamiiForums Tanzania Makelele ya makanisa kwenye makazi siyo sawa kidini, wala kisheria; yadhibitiwe kama makelele mengine

    Makelele ya makanisa kwenye makazi yanakera na kuathiri watu wengi sehemu za mijini, hasa jiji la Dar es Salaam. Aidha makelele hayo yana athari kiafya, kijamii, na hata kiuchumi; kama ilivyo makelele mengine. Na wakati mwingine yana athari zaidi kutokana na kuendelea muda mrefu, bila kuruhusu...
  11. T Kaiza-Boshe

    JamiiForums Tanzania Uenezaji wa ushoga waweza kuwa mbinu mojawapo ya maangamizi ya kimbari

    Ahsante. Nadhani hukunielewa vizuri. Msingi wa hoja yangu ni kwamba ushoga wa mwanaume una madhila zaidi, na kwa mbali sana, kuliko wa mwanamke (msagaji). Mwanamke hata akizaa mapacha kila uzazi hana uwezo wa kuzaa watoto wengi kama ilivyo kwa mwanaume. Nimeilezea vizuri na kutoa takwimu. Na...
  12. T Kaiza-Boshe

    JamiiForums Tanzania Uenezaji wa ushoga waweza kuwa mbinu mojawapo ya maangamizi ya kimbari

    Uko sahihi. Lakini pamoja na kusali tufanye kile tunachoweza kufanya katika ubinadamu wetu kuepusha dhahama. Katika ķisa cha Sodoma na Gomola, angepatikana mtu mmoja safi, angeepusha adhabu jamii nzima. Kuhusu utabili wako wa masharti kwa nchi maskini, siyo miaka mitatu. Huko mbali! Fuatilia...
Back
Top Bottom