JINA LAKO LITANIPA TB.
Mpango chupa za coka, umeleta sokomoko.
mpenzi nawe wataka, chupa yenye jina lako.
nimemaliza maduka, Kibaha mpaka Keko.
Mpenzi badili jina, nisije pata TB.
Nasasa nimeshafika, kiwandani Makondeko.
Makreti napachika, godauni ndo niliko.
Jinalako nalisaka, Nyaminzi mwana...