Recent content by Sam Gidori

 1. Sam Gidori

  Baada ya maka 62 Cuba, haitakuwa na Kiongozi anayeitwa Castro baada ya Raúl kutangaza kujiuzulu Ukatibu Mkuu wa Chama

  Hatimaye, baada ya maka 62, taifa la Cuba litaamka siku ya Jumatatu bila kuwa na Kiongozi wa Nchi anayeitwa Castro! Raúl Castro anatarajiwa kuachia madaraka kama Katibu Mkuu wa Chama, cheo kinachotajwa kuwa na nguvu kuliko cha Rais nchini humo. Raúl, anayetarajiwa kutimiza miaka 90 mwezi Juni...
 2. Sam Gidori

  NASA kumpeleka mwanamke, mtu mweusi kwa mara ya kwanza mwezini kwa bajeti ya shilingi trilioni 55

  Baada ya kutangaza hapa awali kuwa itampeleka mwanamke mwezini kwa mara ya kwanza, Shirika la Marekani la Anga za Juu (NASA) sasa limesema kuwa itampeleka mwezini mtu mweusi katika Mpango wake wa Artemis. NASA imetoa pia ombi la bajeti yake itakayowezesha kumpeleka mwanadamu mwezini kwa mara ya...
 3. Sam Gidori

  Rais wa Brazil kuchunguzwa kutokana na jinsi anavyopambana na corona

  Mahakama Kuu nchini Brazil imeamuru Baraza la Senate kuchunguza jinsi serikali ya nchi hiyo ilivyodhibiti maambukizi ya virusi vya corona, huku ikikataza makanisa kufunguliwa na kuzidisha uwezekano wa kuongeza mvutano baina ya Rais Jair Bolsonaro na mhimili wa mahakama. Uchunguzi huo utahusisha...
 4. Sam Gidori

  India kutafuta njia mbadala ya kufuatilia mawasiliano ya watumiaji wa WhatsApp

  Moja ya sababu zilizofanya mitandao ya kijamii kuaminiwa zaidi na watumiaji ni kutokana na hakikisho la usalama wa mawasiliano kwa kutumia mfumo wa msimbo fiche wa mwisho hadi mwisho (end-to-end encryption). Huu ni mfumo unaoficha ujumbe uliotumwa kutoka kwa mtumiaji mmoja ili usiweze kusomwa na...
 5. Sam Gidori

  Muungano wa Wafanyakazi Uingereza walia na mfumo wa teknolojia wa ufahamu bandia katika ajira

  Muungano wa Wafanyakazi nchini Uingereza umeonya kile ilichokiita 'mwanya mkubwa' katika sheria za ajira na matumizi ya teknolojia ya ufahamu bandia (AI) katika mchakato wa ajira. Kutokana na mabadiliko ya teknolojia yanayoruhusu kuajiriwa au kufukuzwa kazi kwa mfumo wa kompyuta, Muungano huo...
 6. Sam Gidori

  Meli kubwa ya mizigo yashindwa kukwamuliwa katika Mfereji wa Suez kwa siku ya tatu

  Shughuli ya kuondoa meli kubwa ya mizigo iliyokwama katika mfereji wa Suez nchini Misri na kuziba njia kwa vyombo vingine vya maji kupita imeingia siku ya tatu hii leo bila mafanikio yoyote. Jitihada za kugeuza meli yenye uzito wa tani 220,000 na urefu wa mita 400 iliyopewa jina Ever Given...
 7. Sam Gidori

  Utafiti: Pata muda wa kutosha kulala kujikinga na corona

  Katika hali isiyokuwa ya kawaida, watafiti wameonesha kuwapo uhusiano baina ya maambukizi ya corona na usingizi. Utafiti uliofanyika awali ulionesha kuwa asilimia 40 ya watu waliopata maambukizi ya virusi vya corona walikuwa na matatizo ya kupata usingizi. Utafiti mpya unaonesha kuwa watu...
 8. Sam Gidori

  Abiy Ahmed akiri kwa mara ya kwanza uwezekano wa uhalifu dhidi ya binadamu katika mapigano ya Tigray

  Waziri Mkuu wa Ethiopia amekiri uwezekano wa kuwepo kwa matendo ya uhalifu dhidi ya binadamu kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa mapigano katika eneo la Tigray mwezi Novemba mwaka jana. Abiy Ahmed amekiri pia kwa mara ya kwanza, baada ya mamlaka kukanusha mara zote, kuwa vikosi vya Eritrea...
 9. Sam Gidori

  Kiongozi Mkuu wa upinzani Congo-Brazzaville afariki kwa Corona siku ya uchaguzi

  Kiongozi wa upinzani nchini Jamhuri ya Kongo (Congo-Brazzaville) na mgombea wa kiti cha urais amefariki kwa COVID-19 ikiwa ni saa chache tu baada ya vituo vya uchaguzi kufungwa. Guy-Brice Parfait Kolelas alifariki akiwa kwenye ndege akipelekwa nchini Ufaransa kwa matibabu baada ya kuumwa. Saa...
 10. Sam Gidori

  Clubhouse yakabiliwa na ukosoaji kuhusu usalama wa taarifa za watumiaji

  Baada ya kushuhudia miezi kadhaa ya ukuaji wa idadi ya watumiaji, mtandao wa kijamii unaotumia zaidi sauti wa Clubhouse umeanza kukabiliwa na ukosoaji mkubwa hasa kuhusu usalama wa taarifa za watumiaji, na kuifanya kampuni hiyo kuhaha kutengeneza suluhu ya changamoto zake kurejesha imani ya...
 11. Sam Gidori

  Nchi za Afrika zilizowahi kuongozwa na Viongozi Wakuu wanawake

  Mama Samia Suluhu Hassan ameapishwa leo kuwa Rais wa Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia kifo cha Dkt John Magufuli hapo Machi 17. Rais Samia anakuwa mwanamke wa kwanza Tanzania kushika nafasi hiyo. Wafahamu wanawake wengine walioshika nyadhifa za juu kabisa katika nchi zao barani...
 12. Sam Gidori

  Wakuu wa nchi za Afrika waliofariki wakiwa madarakani kuanzia mwaka 1960 - 2021

  Mwaka 2021, Tanzania inaomboleza kifo cha kiongozi wake wa nchi aliyefariki akiwa madarakani, John Pombe Magufuli aliyefariki kwa ugonjwa wa moyo. Hii hapa orodha ya Wakuu wengine wa nchi za Afrika waliofariki wakiwa madarakani kuanzia mwaka 1960 hadi 2021. Mwaka Nchi Kiongozi Sababu 2021...
 13. Sam Gidori

  Nyuma ya pazia ripoti ya chimbuko la Corona inayotarajiwa kutolewa wiki hii

  Baada ya subira ya muda mrefu, hatimaye ripoti ya timu ya wataalamu wa Shirika la Afya Duniani, WHO iliyopewa kazi ya kuchunguza chanzo cha maambukizi ya virusi vya corona inatarajiwa kutolewa wiki hii. Ujumbe huo uliwasili Wuhan mwezi Januari kufanya uchunguzi kwa muda wa mwezi mmoja katika...
 14. Sam Gidori

  Mke wa Rais wa Syria kufunguliwa mashtaka nchini Uingereza

  Miaka 10 tangu kuanza kwa mapigano nchini Syria, Mke wa dikteta na rais wa Syria, Bashar al-Assad, Asma al-Assad anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu na kushawishi uhalifu dhidi ya wananchi wa Syria, mashtaka yaliyofunguliwa dhidi yake nchini Uingereza. Asma ambaye ana uraia...
 15. Sam Gidori

  Facebook kuanzisha mradi wa kufundisha mfumo wake wa ufahamu bandia kwa kutumia video

  Kampuni ya Facebook imesema inaanzisha mradi wa kuifundisha mifumo yake kujifunza picha, video na sauti kutoka katika maudhui yaliyopo katika jukwaa lake. Mradi huo unaoitwa "Kujifunza Kutokana na Video" una lengo la kuufundisha mfumo wa Facebook wa ufahamu bandia (artificial intelligence...
Top Bottom