Australia: Sheria itakayoiwajibisha mitandao ya kijamii kwa watumiaji wasiojulikana kutungwa

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Serikali ya Australia imepanga kutunga sheria itakayolazimu mitandao ya kijamii kuonesha utambulisho wa watumiaji wasiotumia majina halisi watakaochapisha maudhui yenye kuudhi, au kulazimu mitandao hiyo kulipa faini kama fidia kwa madhara yatakayotokana na maudhui hayo ikiwa watashindwa kutoa utambulisho wa watumiaji.

Sheria hiyo mpya inalenga kuiwajibisha mitandao ya kijamii kwa maudhui yanayochapishwa na watumiaji pamoja na kuanzisha utaratibu utakaomwezesha mtumiaji yeyote atakayeudhiwa na maudhui yaliyopo katika mtandao wa kijamii kutoa malalamiko na kutaka maudhui hayo yaondolewe ikiwa yataonekana kumuudhi, kumchafua au kumtishia mtumiaji huyo.

Ikiwa mtandao wa kijamii utakataa kufuta maudhui hayo, mahakama inaweza kuamuru kuonesha utambulisho wa mtumiaji, na endapo mtandao wa kijamii utakataa amri ya mahakama, basi mtandao huo utalazimika kulipa kiasi chochote cha faini kitakachoamuliwa na mahakama.

Akizungumza siku ya Jumapili katika hotuba iliyorushwa kupitia televisheni, Waziri Mkuu wa Australia, Scott Morrison amesema uhuru wa kutoa maoni unapaswa kuendana na uwajibikaji kwa yale utakayozungumza.

“Uhuru wa kutoa maoni hautakiwi kuwaruhusu waoga wanaojificha na kuwachafua au kuwatishia wengine kwa kuwaharibia maisha yao lakini wao wakiwa hawataki kujulikana,” alisema Morrison.

Morrison hakutoa maelezo zaidi juu ya jinsi sheria hiyo itakavyotekelezwa na ni kwa jinsi gani mitandao ya kijamii itaweza kuthibitisha utambulisho wa watumiaji.

Chanzo: RT
 
Hi ije na huku, kumekuwa na vikundi vya kupakazia watu uongo kutokana tu na taarifa za mhusika zinalindwa. Tukiwa na sheria ya vile, wiki tu, uzushi na ujinga mwingi utakuwa umefika kikomo.
 
Hawa Ni democratic, watavikataa Kama kutakuwa na kukiuka haki ya kujieleza
 
Hi ije na huku, kumekuwa na vikundi vya kupakazia watu uongo kutokana tu na taarifa za mhusika zinalindwa. Tukiwa na sheria ya vile, wiki tu, uzushi na ujinga mwingi utakuwa umefika kikomo.
Huku zipo lakini zikitumika utasikia haki za binadamu, mara uhuru wa kuongea... wakati jitu limeingilia uhuru wa watu wengine halafu linataka lenyewe lilindwe na uhuru huo huo
 
Back
Top Bottom