Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 414
Uongozi wa Taliban nchini Afghanistan umesema upo tayari kufanya kazi na nchi zote duniani isipokuwa Israel.
Msemaji wa Kundi hilo, Suhail Shaheen ameliambia Shirika la Habari la Sputnik News la nchini Urusi kuwa Taliban ipo tayari kufanya kazi na Marekani hata baada ya kusubiri kwa miaka 20 kuchukua madaraka tena nchini Afghanistan.
“Tupo katika zama mpya, ikiwa Marekani ipo tayari kurudisha uhusiano wa kidiplomasia na sisi, itakuwa kwa faida ya nchi zote mbili, na kama wapo tayari kuijenga Afghanistan, tunawakaribisha,” Shaheen alisema, akisisitiza kuwa Israel si nchi zilizopo katika orodha yao ya mataifa wanayopanga kushirikiana nayo.
Taliban imetangaza serikali mpya, ikiwahusisha watu walio katika orodha ya kimataifa ya wahalifu wanaosakwa kwa kujihusisha na ugaidi, akiwamo Waziri Mkuu, Mullah Mohammad aliye katika orodha ya waliowekewa vikwazo na Umoja wa Mataifa kwa kujihusisha na utawala wa kikatili kati ya mwaka 1996 hadi 2001.
Chanzo: Times of Israel