Kuna jengo lingine kubwa sana linatarajiwa kuinuka ni maeneo ya ghana upande wa kulia kama unaenda airport .. shimo lililochimbwa kwa ajili ya msingi ni kubwa sana nadhani litapanda hewani nitaleta picha muone
Japo picha haiko vizuri ila kuna ghorofa linanyanyuka hapo mitaa ya nera kwenye mataa upande wa kushoto kama unaenda mjini ukitoka pale mashineni unavuka nyumba moja tu naona wamejenga mpaka daraja kubwa kuvuka mtaro
Stendi ya sgr itajengwa kwenye zile nyumba za polisi station road na hizo nyumba zinavunjwa zote kuna ndugu yangu anaishi pale kanambia wanatakiwa kuhama mapema..ila patapendeza sana hayo maeneo maana kuna mahotel tatizo ni vinyumba vya tanroads hapo
Wanaweka mpka jengo la ccm mkoa hizo taa..pia kenyatta road na nyerere road wanaweka kuna video ilitumwa humu inaeleza kila kitu ngoja nikutumia link usikilize
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.