Hawa wakubwa wanaelewana na wanajua wanachokifanya ktk ulimwengu huu sisi tunabakiwa kuburuzwa tu, mara mafuta yapande bei, mara wakata mwingine watufungie misaada, mara chanjo ya magonjwa mpaka itoke kwao basi ilimradi wanauendesha ulimwengu wanavyo taka wao.
Hawa wakubwa waelewane jamani raia wasiojua mwanzo na mwendelezo na mwisho wa haya yote pamoja na watoto wanateseka sana kwa manufaa ya wakubwa, sijui nani anaweza wanyamazisha hawa wakubwa ktk vita hii. Inaumiza sana kwakweli hizo pande zinazo pigana zina juana wanacho kitafuta na...
Basi tuombe Mungu viongozi wetu watumie kiswahili itatusaidia kukitangaza zaidi jukwaa kubwa sana hilo. Nafikiri tu sijajua kama nipo sawa ktk hilo. Ni katika kukienzi kiswahili chetu.
Hii vita inakwenda kusambaa taratibu na italeta madhara makubwa huko mbeleni, ni jambo la Muda tu maana hata Putin anamarafiki na hawata kaa kimya watasaidiana tu hasa Europe atakavyoongeza misaada u Ukraine .
Kwakweli vita sio nzuri kabisa maana athari inayopatikana ni kubwa mno na wasio na uwezo wa kukimbia au kipigana wanaumia sababu ya wakuu wanao gombana kwa mslahi wanayo yajua wao ni jambo la hatari sana, suhulu ya kudumu inahitajika hapo, sio la kushabikia kabisa hilo. Wakae chini waridhiane.
Mapokeo yanatupelekesha sana bado huku tena kuna AI inafafanua kila kitu basi kizazi kijacho hata kukudhibiti itakuwa shida sana, ni kumwomba sana Mungu tuvuke salama ktk maisha haya ya sasa.
Umesema kwa uchungu sana. ukweli unabakia kuwa ukweli tunapenda kushabikia vya watu vyetu hatuviendelezi wala kuvi tunza na kuvienzi. mapokeo yanatushika akili sana.
Habari za asubuhi ndugu, kuna baadhi ya wafugaji wanasambaza hizo mbegu, Mfano Mavuno ranches kimanzichana 0713 282715. Kimwomwe Ranches kwala 0716787502. Mbogo Ranches mdaula 0784785784. wasiliana na hao wahusika utapata hitaji lako, Mungu akubariki na kukujaalia mafanikio mema ktk ufugaji wako.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.