Mzee nasalimia, wa Kijijini hujambo?
La mgambo likilia, ninajua lina jambo!
Mbiu nimeisikia, sio leo ni kitambo
Unataka kumjua, huyu ndege mwenye mambo
Ndege huyu ni KASUKU!
Ndege huyu ni Kasuku, jina nimelibaini
Si Bata wala si Kuku, hawa ndege wa shambani
Wala si yule Chiriku, wa sauti ya...