Narejea duniani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Narejea duniani

Discussion in 'Utambulisho (Member Intro Forum)' started by Mrimu, Jul 25, 2009.

 1. M

  Mrimu Member

  #1
  Jul 25, 2009
  Joined: Jul 23, 2009
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  (1) Hodi ninabisha hodi, salamu wanakijiji
  Wazee walipa kodi, wa shambani na wa jiji
  Mlioko kwenye bodi, na kamati za majaji
  Narejea duniani, Mrimu wa Herakuli.

  (2) Wa Herakuli Mrimu, imenibidi kurudi
  Kurudi kwa bin Adamu, huenda wakajirudi
  Wakajirudi fahamu, na kuacha ugaidi
  Narejea duniani, Mrimu wa Herakuli.

  (3) Ninatokea Ahera, kwa mizimu wa mababu
  Msije mkanikera, bila kuwa na sababu
  Ni mjumbe mwenye sera, pokeeni matibabu
  Narejea duniani, Mrimu wa Herakuli.

  (4) Syonekani sishikiki, ni mzimu kweli kweli
  Sishiki hiki na hiki, bali ni msema kweli
  Vyote nitavihakiki, ujulikane ukweli
  Narejea duniani, Mrimu wa Herakuli.

  (5) Hamjambo Tanganyika, nchi yangu ya zamani?
  Na Uganda kadhalika, kwa Kaguta Museveni?
  Msije kudanganyika, ufisadi kutamani
  Narejea duniani, Mrimu wa Herakuli.

  (6) Sisi sote ni viumbe, hakuna wangu na wenu
  Mimi hapa ni mjumbe, nimetumwa huko kwenu
  Mkikataa ujumbe, hiyo ni shauri yenu
  Narejea duniani, Mrimu wa Herakuli.

  (7) Wazee wa Barazani, nawaletea salamu
  Wa sasa na wa zamani, kuwaona nina hamu
  Tukutane wahisani, japokuwa kwa kalamu
  Narejea duniani, Mrimu wa Herakuli.

  (8) Mzee Mwana Kijiji, baba u hali gani?
  Kigoma kwenu Ujiji, au Moshi Uchaggani?
  Nataka kuja kuhiji, nyumbani kwenu mwakani
  Narejea duniani, Mrimu wa Herakuli.

  (9) Hongera baba hongera, kwa tungo zako makini
  Za riwaya na ngonjera, za siasa na za dini
  Si Ahera si Kagera, zimefika salimini
  Narejea duniani, Mrimu wa Herakuli.

  (10) Nawe Agustini Moshi, Mwalimu ulo bobea
  Japo hizi hazitoshi, salamu zangu pokea
  Kama bado uko Moshi, naja kukutembelea
  Narejea duniani, Mrimu wa Herakuli.

  (11) Ni kule Kapiri-Mposhi, mpakani natokea
  Nakuja kwa Gari-Moshi, Toka Mkoani Mbea
  Nitapita hapo Moshi, Nikienda Tarakea
  Narejea duniani, Mrimu wa Herakuli.

  (12) Chenye mwanzo kina mwisho, beti hizi nazimega
  Kuna leo kuna kesho, kuna Alfa na Omega
  Salamu zao Kibosho, pia Kenya Kakamega
  Narejea duniani, Mrimu wa Herakuli.
   
  Last edited: Jul 26, 2009
 2. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Just be careful hapa Duniani, sijuwi ulikuwa huka hewani miaka ngapi.

  Karibu duniani
   
 3. GP

  GP JF-Expert Member

  #3
  Aug 20, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  umekaribishwa jamvini, mikono miwili
  jisikie nyumbani, uwe huru kiukweli,
  ruhusa toka moyoni, bila kukujadili,
  karibu duniani, Mrimu wa Herakuli!.
   
 4. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #4
  Aug 20, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280

  jamvini kuna sheria, huna budi zifuata,
  post zitaashiria, kama umezifuata,
  maisha utafurahia, huzuni utazifuta,
  ahera hutafikiria, mawazo utayafuta.
   
 5. GP

  GP JF-Expert Member

  #5
  Aug 20, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  jamvini kuna mengi, makubwa kwa madogo,
  kina mama na madingi, masela na madogo,
  tuma post kwa wingi, ziwe nzito si kidogo,
  karibu duniani, Mrimu wa Hekaruli!.

  mashori ni haba, kina baba wa kumwaga,
  wenye mvuto kimahaba, wajae kwenye vibaba,
  wa mjini si shamba, wao wajaa magaga,
  karibu duniani, Mrimu wa Hekaruli!.
   
Loading...