Wageni kuishi nchini bila utaratibu ni hatari kwa taifa, nchi yetu kwa muda mrefu imekuwa kimya kana kwamba jambo hili ni dogo na halina maana, hapa inatakiwa msako nchi nzima, lakini pia Uhamiaji waliohusika wasiachwe, nao wawajibishwe kama kweli Serikali imekerwa na hili tatizo la wageni holela.