Unakwenda kusikiliza kitu gani? Yaani leo Mgombea Urais wa CCM anaahidi kujenga barabara ya lami yenye urefu wa KM 11 halafu unakwenda kumsikiliza. Huo ni uharibifu wa muda wa kunywa bia
Suala siyo Kenya bali Wandishi wa Habari wa Tanzania wamekosa muendelezo wa uandishi wa habari. Leo hii nakumbuka wangekuwepo akina Jonson Mbwambo, Stan Katabalo (Bingwa wa habari za uchunguzi) pangechimbika lkn leo hii Wandishi wenyewe ndo hawa hata hawaeleweki wanaandika/wanahitaji nini.
Mbowe keshamaliza ngwe yake ya uongozi ndani ya chama, mwacheni apumzike na harakati badala yake kijiti mnacho ninyi endelezeni mapambano. Nampenda sana MZee Mizengo Pinda, yupo kimya kabisa keshamaliza nafasi yake kama kiongozi kawaachia wengine waendeleze pale wao walipoishia
Hapo kwa Rais tumepigwa, aliwahi kuidanganya Dunia kwamba Mbowe anashitakiwa kwa kesi ya uhaini na wahaini wenzie wameshahukumiwa, hizo taarifa anazipataga kwa nani?
Sote tunajua chanzo ni nini hadi kufikia hapa leo Yanga anapogoma kucheza, nakushangaa wewe unayetaka kutubadilisha mawazo kana kwamba jambo limeanzishwa na Yanga.
Hivi kweli Bunge la JMT lijadili kesi ya Lissu!!! Labda mimi ndo sielewi kwamba ''kama kesi ipo Mahakamani haipaswi kujadiliwa na chombo chochote'' Hata hivyo hilo Bunge la Ulaya aliyewatuma kujadili issue ya Lissu ni nani kama siyo kiherehere chao?
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.