Sio kwamba yuko upande wa Rwanda. Jenerali Ulimwengu siku zote yuko upande wa wale wanaoonewa. Ni vizuri kabla ya kuvurumisha maneno tukajaribu kusoma Historia ya Rwanda vizuri tena sio ya kuanzia miaka ya1990 bali kabla ya ukoloni,wakati wa ukoloni na baada ya ukoloni ndipo uje kwenye tukio la...
Nimejaribu kufuatilia "coments" zako unapomzungumzia Nyerere unakuwa na chuki sana naye. Lakini nimejifunza kitu kuwa huenda una mahaba naye makubwa sana na kama ungekuwepo wakati wake huenda ungekuwa nyumba ndogo yake. Kwani baadhi ya wanawake wakiwa na mapenzi kwa wanaume na wanaume na wanaume...
ndugu Tukundane, kawaacha uchi wa mnyama harafu bahati mbaya sana hawataki kuchuchumaa ili kupunguza aibu. Nimemkubali Judge Warioba sana kwa jinsi alivyopangilia hoja zake. Judge Werema ajifunze kwa mzee Warioba na watu wote wenye Taaluma mbalimbali tujifunze kusimamia Taaluma zetu ili...
Ee Mwenyezi Mungu tusaidie. Hivi hawa vijana wenzetu wa Taifa la Tanzania waliopewa dhamana wamelishwa nini hadi kuvurugwa kiasi hiki? January Makamba analinaganisha mfumo wa utawala wa nchi na ndoa? Halafu huyo huyo anataka 2015 tumwamini kumpa uongozi mkubwa wa nchi huku akwa hajtmbui...
kwa hiyo ni halali kufuata maoni ya wabunge wa Bunge Maalum la Katiba 629 kuliko maoni ya wananchi 350,000. Jaribu kutafuta uwiano ni sampuli ipi inayowakilisha wananchi walio wengi kati ya wabunge na hao wananchi waliotoa maoni kwa tume ya Warioba.
Nimejitahidi sana kufuatilia matamko yanayotolewa na viongozi wa chama tawala wanapotetea serikali mbili zilizoboreshwa kuwa ndio suluhu ya kero za Muungano nimeshindwa kuwaelewa kabisa.
Sijui woga wa kuiogopa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar unatokana na nini. Kwa vyovyote vile ilivyo mawazo...
Tume ya Warioba ilisikiliza maoni yako na imeyafanyia kazi, soma ibara ya 188 hadi 193 ya rasimu ya Katiba. Nimepitia na katiba ya Kenya nao wanachombo kama hicho ambacho kimeanzishwa chini ya Ibara ya 79 ya katiba yao. Tofauti ni majina tu lakini majukumu yake ni sawa na yale ambayo rasimu ya...
Hukumwelewa Kinana vizuri, kwa jinsi nilivyomsikia akisema ni kuwa hawapingani na rasimu ya katiba lakini yako maeneo ambayo hawayaungi mkono. Hakuwa tayari kuyasema maeneo hayo huku akisisitiza kuwa ni mapema mno kwani wanaendelea kuisoma rasimu hiyo. Ndipo alipoahidi kuwa ataitisha kikao cha...
Soma vizuri rasimu ya Katiba iliyotolewa Sura ya kumi na tatu TAASISI ZA UWAJIBIKAJI, SEHEMU YA KWANZA, TUME YA MAADILI NA UWAJIBIKAJI Ibara ya 188 hadi 193 utaelewa kile ninachomaanisha. Tume iko huru kabisa kwa mujibu wa rasimu hii na majukumu yake ukichunguza kwa umakini utagundua kuwa yote...
Kwa rasimu hii ya katiba, majukumu ya TAKUKURU yamepelekwa Polisi na kwenye Tume ya maadili na uwajibikaji. Kwa kuwa TAKUKURU tangu mwanzo haikuwa chombo cha Muungano ndio maana haijawekwa kwenye katiba ya Muungano. Labda kama serikali ya Tanganyika itapenda kuendelea nayo kwa upande wake lakini...
Tume hii ni ya kuunda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sio ya kuunda katiba ya Tanganyika kwani kwa sasa Tanganyika haipo, au hata ingekuwepo wasingeunda rasimu ya katiba ya Tanganyika kwani hawana mamlaka hayo kisheria. Kama rasimu hii waliyopendekeza itapita kwenye mabaraza ya katiba...
Mh! too sad for the young man, tumwombee tu ili Mungu asaidie ukweli udhihirike. Vyombo vyetu vya usalama visimame kwenye ukweli. Kama kweli kahusika ijulikane hivyo na kama hajahusika asipewe kesi isiyomhusu. Ni wazi vijana wetu waliojiajiri kwenye shughuli hiyo ya bodaboda hata madereva taxi...
Tuwape pole wananchi wa Arusha na hasa wakatoliki wa Olasiti, kwa muda huu sio vizuri kuweka pilipili kwenye kidonda au kuweka petroli mahali ambako tayari moto unawaka. Tuwe na subira maana ukweli ndio pekee utakaotuweka huru.
Mohamed Said hayo unayoyasema hayalisaidii Taifa kwa sasa wala hayawasaidii waislamu wenyewe.
Kama Nyerere hakutaifisha shule ili waislamu wasome kumbe alifanya hivyo ili wasome akina nani. Wakristo tayari walikuwa na shule zao na mfumo wa elimu uliokuwepo tayari ulikuwa unawapendelea wao...
Nsabhi nashukuru sana kwa kunikaribisha jf, nimechelewa kweli lakini naamini sijachelewa kushindwa kutoa mchango wangu katika jamvi hili la Critical Thinkers.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.