Ndugu zangu, naona wazi kwa macho na akili yangu anguko kubwa sana la CCM kwenye uchaguzi mkuu 2015. Kweli sikio la kufa halisikii dawa. Pamoja na kuwa CCM inaona dalili zote hizi lakini bado haiamki toka usingizi wa kubweteka. CCM inabaki kuwa ndoto
Lazima CCM ikubali kuwa na demokrasia hasa kwa wanachama wake. Wakubali mawazo tofauti ya wanachama wake. CCM itauawa na wana ccm wenyewe na hasa viongozi wasiopenda mabadiliko.
Umechemka mzee. Wewe huwafahamu wana dodoma. Mimi naishi dodoma hapa na nina uhakika ulioongea nao wanasema tu kwa midomo lakini mioyoni mwao wanaipenda ccm. Subiri uchaguzi utaona hata kata moja tu ya dodoma haitaingia upinzani.
Tusiogope kutengwa na Kenya, Uganda na Rwanda. Hawana jipya ila ninachojua ni kwamba EAC itavunjika tena. Maana KENYATTA, KAGAME NA M7 WOTE WANATAKA KUTAMBULIWA.
HONGERA CHADEMA. Matokeo ya Arusha yako vipi mpaka sasa? Naona Makuyuni CCM Magamba wamechukua. Na Tanga kata zote zimebebwa na magamba. SASA TWASUBIRI KWA HAMU MATOKEO YA KATA ZINGINE ZA ARUSHA. Wadau kama mtu ameyadaka basi aweke tuyapate. VIVA CDM
Tumekuwa na serikali inayojali maslahi ya wanasiasa kuliko maslahi ya watumishi hasa sekta ya elimu. Mishahara ya walimu kidogo sana na wanataka walimu wafaulishe. Walimu hawatafaulisha kamwe maana wamejikita kwenye kilimo na biashara kujipatia hela.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.