Katiba mpya ndio inapiga kura ? Suala la msingi ni kujifunza kutokana na makosa na sio kutafuta visingizio. Katiba mpya itafika na uchaguzi utafanyika na wapiga kura ni wale wale. Badilisha mbinu
Inasikitisha ukisema sababu ni jimbo lao maana yake hata uraisi watashinda sababu ni wao wameshinda uchaguzi ulopita. Tuangalie kwa nini wameshinda na kwa nini tumeshindwa.
Unachosema ni kweli, sasa hata mimi ndio naelewa kwa nini kuna watu bunge maalum wanadai kura ya wazi. Naamini kungekuwa na kura ya wazi cdm ingeweza kupata picha halisi ya nani ni mshabiki wa kweli. Nionavyo mimi wengi ni wanafiki anakusifia sana lakini akiwa peke yake anampigia mwingine. Pia...
Lazima mjue haya yaliyojitokeza baada ya kuzima analojia ndi hayo hayo yangetokea 2015. Kwa mtazamo wangu ni bora zaidi kuliko hadi dakika ya mwisho ndio mtu uanze kuhangaika. The earlier; the better
Akienda ccm kanunuliwa, ila akienda cdm kaamua kwa hiari yake na hapo ndipo mnapojidanganya. subirini muone ila tu matokea yakija msianze oo tumeibiwa ila mkishinda ninyi mmeshinda. Kichekesho
Onyesheni hasira siku ya kupiga kura sio humu ndani. Mpira uwanjani ndio kipimo sio. watu aina hii hawakawii kusingizia refa. Fanya mazoezi ingia kwenye kinyang'anyiro sio kusema wahehe wana hasira, wamekutuma ?
Ukiona mtu kazidiwa mara nyingi huwa hana pointi ya maana ila ni kuropoka tu. Waache watu wamchague wanayempenda na sio kuropoka mambo usiyoyajua. Tangaza sera hizo ni dalili mbaya za kushindwa kisiasa. Nenda kapumzike uangalie kwa macho na masikio kama huna la maana.
Na kama ni upinzani basi walianza CUF, na pia mkae mkijua kunapokuwa na makundi tafauti si rahisi kila kundi kukubaliana na jingine hasa kama kuna mitazamo tafauti. Jambo la muhimu ni kukubaliana na pale ambapo hakuna makubaliano basi ni kutafuta maridhiano na sio kutishanaaaaaaaaaaaaaaaaa kama...
Tatizo la watu humu jamvini ni sawa na hadithi ya Nyoka. Wakiambiwa nyoka huyo yuko Morogoro wanasema na apite, nyoka huyo yuko chalinze na apite. basi hadi wasikie nyoka huyo yuko miguuni kwako ndio wanaanza kuhangaika. Inabidi watu humu tusome ishara za nyakati na sio kubeza kila kitu. Huyo...
Mambo mengine ni uzushi wa hali ya juu. Mimi kwangu ITV, EATV, StarTV na nyingine zote nazipata vizuri sana. Hapo mwanzo kulikuwa na tatizo la ITV na StarTv watu walizusha kuwa ITV wanafanya hivyo ili watu waichukie startimes na wanunue digitek kumbe ha hyo haikuwa sawa
Kwani hata hapo mwanzo yanga ilikuwa inavaa nguo kama za tanu ama maana mimi hainiingii akilini ama yanga nayo ilianzishwa baada ya ccm ama ndio ilibadili rangi za jezi ? ama tu kwa vile sasa kiongozi mkuu wa nchi anapenda yanga ? angalieni mtawaponza wengi mkihukumu hivyo
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.