Rais wetu au mtu yeyote, asikosolewe kwa dhihaka bali kwa heshima na hekima. Ujumbe wa maneno aliyoandika unaeleweka kwa kila mtu anayejua kiingereza. Mbona watu wengi wanaoandika "Brocken Swahili" hawambiwi kwa maneno yenye ukakasi kama ya kwako? Tafadhali mkosoeni rais pale amavunja katiba...
Nia ya rais wetu ni kufikisha ujumbe kwa wananchi kwa kutumia lugha rafiki kwa kila Mtanzania anapoliwakilisha taifa. Kiswahili ni lugha rafiki hata kwako mtoa maada. Hata kura za urais alituomba kwa kiswahili na anastahili kutupa mrejesho wa mambo kadha wa kadha kwa kutumia kiswahili.
Daima mkamua jipu huchukiwa na mkamuliwaji kwa sababu ya maumivu anayoyapata. Huyo Trump ni tishio kubwa kwa wenye majipu ya ugaidi, na ndio hasa wanaomchukia.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.