Recent content by kindokicha

  1. K

    JamiiForums Tanzania Bosi wa UNDP ashauri UKAWA warudi bungeni

    Siyo kweli kwamba UNDP ni mtumishi was USA. Tatizo waandishi wetu hakumwelewa huyu mama. Yeye kaongea kidiplomasia wenyewe wakaripoti kinyume!!
  2. K

    JamiiForums Tanzania Maandalizi ya Muungano: Wanajeshi washuka na parachute

    Hii imekaa safi sana! Tuna kila sababu ya kujivunia JWTZ.. Linatimiza majukumu yake kwa weledi na uzalendo!!
  3. K

    JamiiForums Tanzania Mbowe: Hakuna popote UKAWA walipomtukana Mwl Nyerere, Msitulishe uongo wenu!

    Hii siyo sawa. Tunaweza kuwa na misimamo na hoja kizani lakini ni busara kuzitoa kwa hali inayojenga utanzania wetu siyo kwa njia ya kubomoa! Je kuzidi kuchochea hisia hasi za kikabila na vitisho ndiyo njia nzuri ya kuchangia mijadala mizito ya kitaifa? Mbaya zaidi kujaribu kutoa twasira kuwa...
  4. K

    JamiiForums Tanzania Maaskofu 32 Katoliki wataka Tume ya Warioba iheshimiwe

    Tafadhali jifunze kujenga hoja. Hueleweki! Aidha huna uhakika na ulichoandika au unasukumwa zaidi na ushabiki au unafiki wa aina fulani. Kumbuka jukwaa hili linatembelewa na watu wenye akili zao....
  5. K

    JamiiForums Tanzania Baada ya kutoka bungeni - hii ndio post ya Julius Mtatiro... Vitisho makanishani

    Ni vizuri viongozi wetu kisiasa hasa walio madarakani wakatambua uzito na umuhimu wa dhamana waliobeba kwa niaba ya Watanzania. Wanatakiwa mara zote wajiepushe na kauli zinazobomoa umoja na mshikamano wa kitaifa. Haipendezi hata kidogo kiongozi kushadadia mambo hasi tena mbele ya umati wa watu...
  6. K

    JamiiForums Tanzania Dar yageuka `Sodoma` kwa ngono za wazi hadharani

    Well said! Ni vizuri kuikomesha biashara hii haramu inayodhalalisha heshima na utu wa mwanadamu! Polisi waachane kutumia mbinu za kizamani. wawashughulikie zaidi wale wanaoifanya biashara hii kushamiri ambao ni wanaume.... Wanaume wengi wanachelea sana kuaibika. Wakitiwa msukosuko dada poa...
  7. K

    JamiiForums Tanzania Malisa akataa ubunge

    Inaudhi sana tena sana watu karne ya 21 tunazungumzia ukabila tuu!! Tubadilike....
  8. K

    JamiiForums Tanzania Waziri apigwa marufuku kutembelea jimboni kwake, katibu CCM ahaha kutafuta suluhu

    '..GODSONI MBAGA amewaomba wananchi kumchagua kwa kishindo mwaka 2015 kupitia CHADEMA kama akipewa ridhaa kuipeperusha bendera ya chama Same MAGHARIBI. Pia amewataka makada wa CCM wanaorubuniwa kwa fedha za walipa kodi ili waendelee kuwa watumwa wa CCM kuepuka tabia hiyo kwani ni dhambi na...
  9. K

    JamiiForums Tanzania UDINI: Uchafu Chini ya Kapeti tunajidanganya wasafi - Zitto

    Hebu kama watanzania tuelewe maana halisi ya UDINI; tafsiri yangu ni kuwa; ni ubaguzi na utayari kwa kutenda lisilo jema kwa binadamu mwenzako kwa sababu tu si wa imani yako. Tujiulize, je hivi ndivyo imani zetu zinataka? Na kama sivyo hatuoni kuwa tunapotoka kwa kuwasilikiza na kukubali...
  10. K

    JamiiForums Tanzania UDINI: Uchafu Chini ya Kapeti tunajidanganya wasafi - Zitto

    Well said! Hakika tukiendelea kutowakemea na kutowathibiti kwa nguvu zote wanaoendekeza na kuupalilia udini kwa maslahi na sababu zao; taifa letu litasambaratika na kuwasababisha maafa makubwa kwa kila mmmoja wetu. Wenye dhamana na mamlaka ya kuhakikisha nchi yetu inajengeka kama mahali bora pa...
  11. K

    JamiiForums Tanzania Waziri Nchimbi alaaniwa na Wazanzibari! Maalim Seif amjia juu...

    Hakika itashangaza sana endapo huyu jamaa mtoa mada asipotakiwa kutoa ushirikiano kusaidia uchunguzi. He/she seems to have some leads....Atakiwe na vyombo vya usalama kueleza yale anayojua kuhusu kadhia hii...
  12. K

    JamiiForums Tanzania Buseresere: Mapigano makali yaibuka kati ya waislamu na wakristu!

    Ndugu Watanzania wenzangu, zinahitajika chehe tu kuichoma nyumba. Nyumba yetu sote ni Tanzania lakini inasikitisha jinsi baadhi ya watu wanavyozidi kuchochea chuki za kidini. Yanayotokea hivi sasa kule Geita ni kiashiria kibaya kwa siku za usoni kama sote kama taifa tutashindwa kuweka tofauti...
  13. K

    JamiiForums Tanzania TANZIA: Askofu Mstaafu Amedeus Msarikie afariki dunia leo alfajiri

    We celebrate your life for what you did for the Church and Tanzanians. You served with all humility and christian love. Through your deeds and words you made Jesus endless love be felt by many, belivers and non-believers. May the merciful and gracious Lord grant you a place among his saints...
  14. K

    JamiiForums Tanzania Watumishi wa serikali wagwaya kutembea na katibu kwa kuhofia kuhisiwa wako CHADEMA - MOSHI MUNICIPAL

    Uoga ni adui mkubwa wa maendeleo yetu. Mtumishi wa umma anayeogopa kusema na kuwa na ujasiri wa kusimamia kilicho sahihi na haki ana kasoro kubwa ktk utendaji wake na hawezi kutetea maslahi ya umma. Wafanye tafakari, wajue haki zao waondoe uoga!:A S angry:
  15. K

    JamiiForums Tanzania Deo Filikunjombe: Tanzania sio mali ya CCM

    Ukweli siku zote huweka mtu huru. Tanzania ni zaidi ya chama/vyama. Uzalendo, uadilifu na uwajibikaji kwa umma wa watanzania ndivyo vinavyohitajika. Bahati mbaya sana haya yanapelea ua kukosekana kabisa kwa chama tawala. Deo is an exception........ Keep it up.:happy:
Back
Top Bottom