Bosi wa UNDP ashauri UKAWA warudi bungeni

Bosi wa UNDP ashauri UKAWA warudi bungeni

Kilicholeta kutoelewana ni mfumo wa muungano, serikali 2 au 3. UNDP wao wana mfumo gani wa muungano? Watakuwa hawana akili kama wataenda nje ya rasimu iliyopatikana kutoka kwa wananchi.
 
Ushauri huu naona asubiri kama nchi yake alikotoka wanataka kubadili katiba aende akautoe kwao. This is Tanzania na sisi watanzani ndiyo tunajua maumivu yaliyosababishwa na yanayoendelea kusababishwa na serikali la wala rushwa. mafisadi na mabepari wanaotaka kufanya wengine watwana maana hata vyeo vimeshakuwa vya kupokezana kama vile vya machifu. Mama wewe unapokea mshahara kwa madola ambao mwezi mmoja ni zaid ya mishahara miaka ishirini ya mtumishi wa serikali achilia mbali wananchi wanaoishi kwa mlo mmoja kwa siku na siku nyingine hawali kabisa. Acha kabisa siasa zetu mama.
 
..JK kageuza hii nchi ombaomba kiasi kwamba kila mtu anayesaidia TZ anaona ana haki ya kutuambia nini cha kufanya ili kupambana na matatizo yetu....haya anayosema huyu mama wa UNDP ni matokeo ya nchi hii kugeuzwa ombaomba wa dunia hii......ni mbaya zaidi pale watawala wanaposhabikia mambo haya.....enzi za Nyerere upuuzi kama huu haukukubalika kabisa.....watawala wa leo wanajifanya kumuenzi Nyerere ...lakini wanashindwa kutenda kama yeye......inasikitisha sana.....
 
samahani mtanisamehe kwa kuongea hili japo nje ya mada make nimepost naona moods hawakuipenda wakaitoa,wazungu wanajaribu kutuondoa sisi weusi ili wabaki na wanyama kwani wanapata pembe,ngozi na kwato tofauti na sie uwepo wetu hauwanufaishi ndo maana wanahamisha watanzania waachie makazi yao kisa wanyama ...hivi kumbe UNDP nako kuna wajinga kama huyu mama
 
Nchi hii ni yetu si ya UNDP watuache kabisa
 
Trust me. Wanaijua sana tu. Wakoloni huwa ni wanafiki kuliko maelezo. As long as wanapata kila wanchotaka wataendelea kuwa sifu kwa mapambio ya kila aina. Mkitaka kujua ni kiasi gani wanawafahamu, nyie wageukeni, halafu muone ushahidi wanaokuja nao wa kuwabomoa! Hawa siyo watu. Kuna wakati huwa nataka kuanza kuamini kuwa kuwa "mru mweupe" ni kuwa na kasoro kimaumbile. I mean huwa nakaribia kufikiri kuwa viumbe sahihi walikuwa "watu weusi" ..... but I don't believe in that or any other theory, nadhani wote ni binadamu ila wengine ni wanafiki na wamekosa ubinadamu ndani yao, kwa hiyo, ni sawa na migomba inayotembea!
Mwandishi kammisquaote. A diplomat wana kauli na lugha yao; au kaongea kiingereza waandishi hawakumwelewa!
 
Kilicholeta kutoelewana ni mfumo wa muungano, serikali 2 au 3. UNDP wao wana mfumo gani wa muungano? Watakuwa hawana akili kama wataenda nje ya rasimu iliyopatikana kutoka kwa wananchi.

Ili kujua UNDP inaunga mkono 2 au 3, kwanza kabisa ni kuchunguza USA ina msimamo gani? UNDP huwa inatekeleza matakwa ya USA. US wakitaka serikali 2 au 3 basi itakuwa hivyo. UNDP ni mtumishi tu.
 
Mwandishi kammisquaote. A diplomat wana kauli na lugha yao; au kaongea kiingereza waandishi hawakumwelewa!

Sijui sana. Ila kama una quote sahihi ni vizuri ukatupia hapa kuondoa utata. Ila msimo wangu unabaki palepale kuwa Hizi ni siasa za Tanzania wakae kimya wawaachie Watanzania, na pia watu weupe ni wanafiki sana. Hata bila quote yoyote huo ni msimamo wangu.
 
Ili kujua UNDP inaunga mkono 2 au 3, kwanza kabisa ni kuchunguza USA ina msimamo gani? UNDP huwa inatekeleza matakwa ya USA. US wakitaka serikali 2 au 3 basi itakuwa hivyo. UNDP ni mtumishi tu.

Siyo kweli kwamba UNDP ni mtumishi was USA. Tatizo waandishi wetu hakumwelewa huyu mama. Yeye kaongea kidiplomasia wenyewe wakaripoti kinyume!!
 
Sijui sana. Ila kama una quote sahihi ni vizuri ukatupia hapa kuondoa utata. Ila msimo wangu unabaki palepale kuwa Hizi ni siasa za Tanzania wakae kimya wawaachie Watanzania, na pia watu weupe ni wanafiki sana. Hata bila quote yoyote huo ni msimamo wangu.
Upo correct Elly B, watu weupe ni wanafiki sana na dharau juu.
 
Inasikitisha mkubwa kama yeye (Clark)kwa nafasi yake anaweza kuchukulia mambo kijujuu hivyo. Ukisikia anatusifia katika chaguzi zilizopita wakati hatuna tume huru, wakati chaguzi zilizopita zimelalamikiwa kiasi kikubwa na pia katika jitihada za kuondoa umaskini unaelewa wazi haw nin walewale ambao kwa taarifa za upande mmoja ni tosha hawataki kuingia ndani zaidi. Nafurahi kwani UKAWA wamemuelewa vizuri.Angetaka ukweli angenongona na Dr Asha Migiro huku ground kidogo ni tofauti na kule UN, theory haziapply mara nyingi
 
SIKUJUA KAMA HUYU MAMA ANAPIGA KAMPENI YA KUHALALISHA USHOGA DUNIANI sasa mleta mada tupe sababu ya kwa nini ukawa au watanzania tumsikilize anachotushauri
 
...Neo colonialism.
Hawa ndio wanauvuna rasilimali za Tanganyika, hawawezi kukubali ifufuke !
 
Nashauri UKAWA wamuandikie barua kumchana na kumjulisha kuwa watarudi BMK endapo bunge hilo litaanza kujadili rasimu iliyowasilishwa na tume na pia ccm wataacha matusi, ubaguzi na vitisho
 
Nashauri UKAWA wamuandikie barua kumchana na kumjulisha kuwa watarudi BMK endapo bunge hilo litaanza kujadili rasimu iliyowasilishwa na tume na pia ccm wataacha matusi, ubaguzi na vitisho

Inawezekana hajui wanajadili katiba gani. Na hajui ni Kwanini UKAWA walitoka nje. Inaonekana amesikiliza upande mmoja i.e Rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM.
 
Bosi wa undp yupo hapa katokana no uongozi mbovu tulionao tu, venginevyo hatumuhitaji tunajitosheleza kabisa,
Anayasema haya kulinda ajira yake tu
 
Back
Top Bottom