Kwanza kabisa nilishangaa sana namna baadhi ya Vyombo vya Habari vilivyoliwasilisha suala la noti mpya. Kwa namna Mh. Rais alivyozungumza kuhusu suala hili, sikutaraji kabisa Vyombo vya Habari hivyo kuupa Umma tafsiri isiyo ya kweli katika suala hili la noti mpya: Mhe. Rais alizungumza mambo ya...
Ni maombi yangu kwa Mwenyezi Mungu kuwa Mheshimiwa apate fursa ya kuusoma ushauri wako huu, ndugu Msambichaka Mkinga. Nashukuru sana kwa kupata muda na kuandika ushauri huu mzuri.
Huwa nikiona 'uzi' wako, nakasirika sana kwa unafiki wako. Na, kwa kweli huwa najilaumu sana hata kwanini nilikuwa nakuheshimu mtu kama wewe. Lakini, muhimu ni kuwa sasa rangi yako halisi inajulikana.
Ni vyema ukajifunza kukubali kukosea ili ujirekebishe; sasa umekwepa neno hilo kuwa siyo tusi (ijapokuwa ukweli ni kuwa hilo ni tusi), je na lile lililofuata baada ya hilo?
Kwa kweli, watu tumetofautiana sana; sasa wewe ndugu, kulikuwa na haja gani ya kutoa maneno machafu kiasi hicho eti kwa sababu tu umetofautiana kimawazo na mleta hoja?! Ndugu, nafikiri ilikuwa ni vyema uandike mawazo yako kueleza kwanini unafikiri mawazo ya mleta hoja hayana mashiko.
Ebwana, nakuunga mkono sana kwa hoja yako hii. Nina uhakika kabisa Mh. Rais ana nia njema sana na Nchi yetu na nina uhakika kwa kasi yake tutafika mbali sana; hata hivyo, mawazo yako haya uliyoyaandika hapa jamvini hakika ni ya msingi sana. Ninaamini ipo siku Mh. Rais atayafanyia kazi.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.