Kauli Fupi ya Kuudhi: Upepo wa Jana Hausukumi Meli Leo

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,739
40,863
Salama humu, tatizo moja ambalo wapo ambao labda hawataki kulifikiria ni kuwa bado watu wanafikiria hii ni baada ya uchaguzi wa 2010. Kuna kitu kimebadilika sana katika fikra za Watanzania na kitu hicho naamini kinabadilisha kabisa mijadala ya kisiasa. Binafsi sasa hivi naangalia mambo kwa mwanga tofauti zaidi; wapinzani hawawezi tena kutegemea upepo wa jana kusafiria leo.

MMM
 
Kwa nini unafikiri hii ni kauli ya kuudhi? Sidhani kama ukweli unaudhi bali unaumiza tu kwa wale ambao hawataki kuukubali. Ulichoeleza ni ukweli wala sioni maudhi hapo.
 
Wote tuliona yaliyotokea; kumbe kuna kanuni ambazo wengine tulitarajia wao wazijue zaidi. Lakini siyo hivyo tu; walipokula kiapo cha kulinda Katiba wakubali kulinda yote siyo tu inapowafaa. Ndio maana binafsi kama kweli wanaamini katika kutokutii na kuona kuwa wameonewa na hawawezi la maana ni kujiuzulu. Huwa nalirudia mara kwa mara hili. Usipinge tu ukapinga halafu ukataka kuendelea. Sasa kama kanuni za mchezo mtu unazijua lakini unaamua kuzivunja kanuni zile zile zikikuadhibu vipi utasema zimekuonea unless uamue kujilipua kweli kweli? Juzi tumesikia Waziri wa Israeli huko ambaye hakubaliani na Netanyahau kaamua kumwagia manyanga kumpinga. Siyo anampinga halafu anataka kuendelea kuwa waziri! Hii ni kanuni muhimu sana.

Lakini hakuna njia nzuri zaidi ya kutaka kufanya unachotaka kufanya kama kushinda uchaguzi. Walioshinda uchaguzi ndio wanatuburuza na ukwlei ambao wengine hawataki kusema ni kuwa mwaka jana ushindi tumewapa wenyewe tena kwa kuwabebea! CCM mwaka jana hata kama ingeshinda urais kwa kweli kabisa isingepaswa kushida Ubunge. Lakini Watanzania waliamua na kuona kilichotokea hata waliokuwa na mawazo ya kuupigia upinzani kura waliamua kubadili mawazo pale wenzetu walipoamua kubadilika. Walipobadilika na wao wakabadilika.!
 
Hichi kizee zamani kikitupia uzi ilikuwa lazima mtu ufungue kusoma na kilikuwa kinapendwa sana mi mmoja wapo! Ila kwa sasa kinapuuzwa tu na chenyewe kimeziba masikio kabisa!! Bora mkuu amalize hizi teuzi zilizobaki watu warudi kwenye akili zao!!!
 
Upinzani unahitaji strategic re-alignment...vinginevyo watakuwa wanajaribu kutumia stamp za zamani kutuma barua.
Unanikumbusha kipindi cha kufoji, halafu barua yako ikikurudia unalalama kwelikweli....! Na mara nyingine unapata barua, ukijaribu kufoji unakuta haifojiki kwa sababu kumbe tayari ilishafojiwa....! Sasa chukulia unampatia mtu akufojie ukiamini ndiye mtaalam, halafu akaharibu...! Lazima anunue stamp, la sivyo mtaamuliwa...!
 
Wapinzani wa kweli hapa Afrika ni BASHE,ZITTO ,UKAWA na Wapinzani wa Bunge la Africa kusini/kenya.....sitashangaa siku nikiona ngumi bungeni ,kwasababu najua kinachoendelea sasa ni hizi serikali hazisimamiwi na mabunge haya ya jumuiya ya madola bali serikali ndiyo inayo simamia mabunge haya.
WABUNGE HAWA WA UPINZANI NDIO HUANZISHA MADA ZA UFISADI LKN KATIKA ZAMA HIZI SERIKALI HIZI ZINAKUMBATIA UFISADI HUU
Ref:Lugumi/bunge live si hoja za kubeza.
Ref:Zuma kutumia hela ya serikali kurekebisha nyumba yake.
 
Wote tuliona yaliyotokea; kumbe kuna kanuni ambazo wengine tulitarajia wao wazijue zaidi. Lakini siyo hivyo tu; walipokula kiapo cha kulinda Katiba wakubali kulinda yote siyo tu inapowafaa. Ndio maana binafsi kama kweli wanaamini katika kutokutii na kuona kuwa wameonewa na hawawezi la maana ni kujiuzulu. Huwa nalirudia mara kwa mara hili. Usipinge tu ukapinga halafu ukataka kuendelea. Sasa kama kanuni za mchezo mtu unazijua lakini unaamua kuzivunja kanuni zile zile zikikuadhibu vipi utasema zimekuonea unless uamue kujilipua kweli kweli? Juzi tumesikia Waziri wa Israeli huko ambaye hakubaliani na Netanyahau kaamua kumwagia manyanga kumpinga. Siyo anampinga halafu anataka kuendelea kuwa waziri! Hii ni kanuni muhimu sana.

Lakini hakuna njia nzuri zaidi ya kutaka kufanya unachotaka kufanya kama kushinda uchaguzi. Walioshinda uchaguzi ndio wanatuburuza na ukwlei ambao wengine hawataki kusema ni kuwa mwaka jana ushindi tumewapa wenyewe tena kwa kuwabebea! CCM mwaka jana hata kama ingeshinda urais kwa kweli kabisa isingepaswa kushida Ubunge. Lakini Watanzania waliamua na kuona kilichotokea hata waliokuwa na mawazo ya kuupigia upinzani kura waliamua kubadili mawazo pale wenzetu walipoamua kubadilika. Walipobadilika na wao wakabadilika.!
Mwanakijiji nakuheshimu mno lakin nahisi kuna kitu si sawa.
Kwanza nakiri ya kuwa Raisi wabgu ni Magfuli whether nilimchagua au sikumchagua lakini madam kaapishwa huyu ndiye Rais wangu.
Tangu Raisi huyu ameingia madarakani amekuwa ni mtu wa kujipambambanua kama asiyekubaliana na mengi yalifoyafanya na awamu iliyopita.Hili lilinishangaza sana nikukumbuka alivyokuwa akimsifia Kikwete katika uzinduzi wa barabara.
Kwa nayofanya leo kwa maneno na vitendo naamini ya kuwa alikuwa hakubaliani na Kikwete kwa asilimia zaidi ya 95%.
swali,ni kwa nini hakujiuuzulu wakati ule???
Kama kawaida wapambe wanasema angejiuzulu asingeipata hii nafasi na maana yake ni kuwa alikuwa ndani ya serikali akifanya asiyoyaamini.
Kujiuzulu wabunge hakutasaidia nchi lakini kama una mawasiliano na mkuu ana uwezo wa kuvunja bunnge na kuitisha uchaguzi mpya.I am sure CCM itashinda kwa 98% na hili lingekuwa jambo bora zaidi.
Asubuhi njema.
 
Salama humu, tatizo moja ambalo wapo ambao labda hawataki kulifikiria ni kuwa bado watu wanafikiria hii ni baada ya uchaguzi wa 2010. Kuna kitu kimebadilika sana katika fikra za Watanzania na kitu hicho naamini kinabadilisha kabisa mijadala ya kisiasa. Binafsi sasa hivi naangalia mambo kwa mwanga tofauti zaidi; wapinzani hawawezi tena kutegemea upepo wa jana kusafiria leo.

MMM
Huwa nikiona 'uzi' wako, nakasirika sana kwa unafiki wako. Na, kwa kweli huwa najilaumu sana hata kwanini nilikuwa nakuheshimu mtu kama wewe. Lakini, muhimu ni kuwa sasa rangi yako halisi inajulikana.
 
Kuna watu wamelirudisha nyuma taifa hili kidemokrasia. Wamewatia watu unyonge, watu wameacha kuamini kwa wanasiasa. Wale waliokuwa wakiwaamini sana tena sana, wale waliokuwa wakisema huku wametokwa macho, mindai ndai na mishipa ya shingo imewatoka kutuaminisha kile walichokuwa wakikisema, leo ni wale wale wameyabadilisha yale maneno. Tena kwa mtindo ule ule wa kutoa macho na mishipa ya shingo kutuaminisha wanachokisema kikipingana na kile walichokisema awali. Hata wakitoka nje, hawaaminiki tena kwani walitoka nje kutuaminisha yale ambayo leo wanayapinga. Wametufanya watu wote tuliokuwa tunapigia kelele demokrasia na kuukemea ubadhirifu kuonekana mahayani. Kama kuna watu wigo wao wa kufikiri umejengwa na jina la chama hao wataendelea, lakini wenye tafakuri pana na akili timamu, wamewatambua maadui wa demokrasia wa taifa hili ambao kwao siasa ni 'kaole' tu na wala si maisha ya watu.
 
Back
Top Bottom