Hizi siasa za Tanzania ya leo zinatia kichefuchefu. Mtu unajigamba kufanya maendeleo lukuki , lakini bado unahangaika kuchafua watu na kuwatisha......!
Inasikitisha sana hapa Tz hakuna maendeleo yoyote tunafanya yenye maana katika karne ya Leo zaidi ya kupigana vijembe kama waimba taarabu, si serikali si vyama vya siasa, si wananchi wenyewe. Tupo kama tumerogwa vile. Hebu angalieni wenzenu Kenya wako vipi [emoji116] [emoji116] [emoji116] tuamke...
Kimsingi kila utawala una mazuri na mabaya lakini mazuri yako haya tufanyi kuacha kuyaona mabaya na kuyakemea lazima tuseme kwa sauti kubwa pale serikali inapo kosea kwani hatukuichagua kuja kukosea tumeichagua kuja kututoa katika matatizo yaliyo kuwepo na yaliyo tengenezwa na watangulizi wake...
Tunacho kionya hapa ni lugha chafu ambazo halingani na Utanzania wetu, kwahiyo kama anafanya unachokipenda anahaki ya kututolea matusi na kejeli ??? Anapo omba tumuombee je Mungu tunaye muamini anapenda dharau na matusi ?? Anacho kifanya anatimiza wajibu wake kama Rais wa Nchi na Anawajibika...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.