Rais Magufuli: Nilitaka kwenda kupiga kura lakini nikiwa hapa kanisani nimesikia mgombea amepita bila kupingwa hivyo nampongeza

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,897
141,832
Rais Magufuli amesema alikuwa anataka kwenda kupiga kura lakini amesikia katika mtaa wao mgombea amepita bila kupingwa.

Rais Magufuli amesema hayo akiwa ibadani katika Kanisa katoliki la mt Imaculata, Chamwino Dodoma.

Dr Magufuli aliwataka waumini ambao uchaguzi unafanyika katika mitaa yao wakawachague wagombea wanaowapenda kwani Maendeleo hayana vyama.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Thubutu anavyopenda kamera, sema kaona watu hakuna aibu atajipanga na nani kwenye foleni? Wewe hushangai leo waziri mkuu, makamu wa rais hawaonyeshwi wakipiga kura? Aibu hamna watu.
 
Utapeli gani?!
Kiongozi akikosa, amekosa tu, kumpamba ni kumdanganya. Rais ametukosea sana Watanzania kwa kuharibu uchaguzi wa kidemokrasia kisha kututeulia wenyeviti wa mitaa, vitongoji na vijiji.

Anahitajika nabii Nathan kumwambia Mfalme ukweli machoni: "Mtu huyo ni wewe."

Kusimama mbele ya madhabahu na kusema aliyoyasema ni kumdhihaki Mungu huku akijua kuwa alichofanya kinahitaji toba ya dhati.
 
Back
Top Bottom