Nina bahati ya kukufahamu kitambo kidogo tukiwa bado watoto wadogo pale kawe.. Najua uwezo wako na naamini utaweza kuwa kiongozi bora kabisa katika taifa hili.. Wish you best of luck Mpoki!
Rgds
Ditto
All the best kaka!
Mchambuzi
Labda kama sijakuelewa vizuri, lakini kwa uelewa wangu mdogo Zitto alivuliwa uongozi na CC na amekata rufaa. Nafikiri kikao kinachohusika na hii rufaa kitapangwa na kuisikiliza. Ishu aliyoombwa kuitolea maelezo inahusu ni kwanini asivuliwe uanachama (kumbuka bado CC ina-uwezo wa kumhoji na...
Nguruvi3 mpaka sasa sitaki kuamini kama ule waraka pamoja na hilo bandiko uliloliweka hapo linatoka kwa kijana msomi na aliyebobea katika siasa. Siwezi kubishana nae sana maana kiusomi, ni mtu aliyeniacha kwa mbali lakini kwa uelewa wangu mdogo, naona mapungufu mengi sana katika namna...
Kaka Pasco
Kwenye suala la uchanga kisiasa, hilo naliafiki 100%. Lakini pia, chama hakiwezi kukua bila kupitia changamoto za aina hii. Changmoto za aina hii huwa na results za aina mbili, kuvuka salama na kuwa chama chenye mvuto zaidi kuliko ilivyokuwa hapo mwanzo; au kufa kibudu kama...
Nakubaliana na wewe kabisa katika suala zima la mapungufu katika katiba yetu ya nchi especially katika hicho kipengele cha kumuondoa mtumishi wa umma kwa manufaa ya chama.
katika suala hili, naomba nitofautiane na wewe kidogo. Chama kinahitaji kuonekana kama ni taasisi yenye wafuasi wenye...
Nguruvi3 Mchambuzi
Nakubaliana na uchambuzi wenu katika vipengele vyote kuhusiana na mapungufu kwenye huo waraka. Pia nakubaliana na nyie kwenye maeneo ambayo waraka umegusia ambapo kusingekuwa na nia mbaya, huenda hayo mapungufu yaliyoainishwa yangeweza kukisaidia zaidi chama katika kukijenga...
Seriously?! Nafikiri hawa jamaa wanaona bungeni ni sehemu ya kufanya mzaha.. Or possibly upeo wake unamtuma kwamba hiyo inaweza kuwa sababu ya shillingi kuporomoka..
Watu wa kusini si kwamba wanadai gesi isisafirishwe ila wanahoji wananufaika vipi kwa rasilimali iliyoko kwao inayochukuliwa kwenda kuwanufaisha wengine.
Hilo ni suala ambalo viongozi hawawezi kukwepa kulielezea.. Lazima Mtwara wanufaike kwa rasilimali zao kabla ya kupelekwa sehemu ingine...
Kuna ubaya gani wa kurekodiwa kama kulikuwa hakuna la siri mlilokuwa kuwa mnaliongelea? Kungekuwa hakuna kitu cha kufanya mrekodiwe, hakika asingeweza kufanya hivyo maana hiyo habari isingeuzika.. Mmekuja na utetezi wenu lakini hauna mashiko.. Nendeni mkajipange upya!
Yericko Nyerere Well, hata mie nimesikitika sana kwa hili alilolianzisha ndugu yetu msemaji wa chama tawala.. Nahisi sasa chama tawala kinapoteza focus na kujiendesha kama chama cha upinzani.. Kuna mengi sana wananchi wanatamani kuyasikia kuhusu maendeleo kuliko hili suala la Dr. Slaa na kadi ya...
Sina hakika kama suala la wapi hiyo sera ilizinduliwa ndio hasa chanzo cha kukwama kwa hii sera kuenea na kukubaliwa ndani ya jamii. Shida ipo katika wale viongozi kushindwa kuliongelea kwa wananchi aidha kwa kutokuielewa vizuri hii sera au uoga tu kwamba na yeye ataitwa mbaguzi.
Matola hakika umegusia vipengele vyote muhimu kuhusiana na hii sera.
Umenigusa zaidi ulipogusia sera ya CCM ya "Kilimo Kwanza". Nafikiri CCM nao walipofeli kwenye hii sera ni kutowashirikisha wananchi vya kutosha katika kuielewa na kuweza kwenda nayo sambamba.. Matokeo yake tumetumia fedha...
Wanabodi
Nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa siasa za hapa nyumbani na kwa hakika kiwango cha siasa tunachofanya kwa sasa kina utofauti mkubwa sana ukilinganisha na miaka 20 iliyopita. Siasa za sasa zimejaa ushindani na vijembe vya hapa na pale ambavyo pamoja na kuleta burudani na hamasa, pia...
Mchambuzi naona umeongelea kitu ambacho vijana wengi tunashindwa haswa haswa washabiki wa chama tawala. Tumezoea kujipendekeza na kuongea vitu hata kama vitu hivyo vinapoteza muelekeo sio tu wa mtu binafsi pia chama au taasisi kwa ujumla wake. Hii imenikumbusha kisa cha mfalme aliyekuwa uchi...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.