Hili mbona lipo wazi muda mrefu sana mkuu Bams,adui wa Tanganyika ni watanganyika wenyewe.
Tunaishi na jamii ya kinafiki ambayo haija wahi tokea kiasi kwamba mpaka una shangaa hawa watu akili zao zipo timamu kisawa Sawa.
Huo ndo ukweli mchungu ambao makada wengi wa chama Cha mapinduzi hawataki kuusikia, watanzania tumelea mfumo wa hovyo wa kiutawala wenye kulinda maslahi ya viongozi na sio umma Leo hii viongozi wamekuwa wakubwa kuliko umma ulio wapa madaraka mwisho wanauza Mali ya umma bila wasi wasi na hofu...
Katiba mpya ndo moyo wa taifa hili ifikie wakati tuweke utofauti wa itikadi pembeni bali kuangalia maslahi mapana ya taifa.
Inasikitisha kuona kwamba Mali zilizopo Tanganyika zinauzwa na wageni uku wenye mali tukishangilia kwa kusifu na kuabudu ili kumfurahisha mwenyekiti wa chama na kikundi...
Kuna bwana kasha wahi sema kwamba wanasheria wengi wa serikali ni goigoi na hii ni kutokana na ukweli kuwa wanapo shindwa makesi hukimbilia kubadilisha Sheria badala ya kukata rufaa,sasa wakikutana na wanasheria nguri kutoka nje ambao hawa tegemei mfumo kuwabeba Wana shindwa.
Kaburu Botha alisha wahi sema kwamba "mwafrika hawezi kujitawala"
Ifikie muda tukubali kwamba waafrika siku tukishimda vita juu ya ubinafsi tutakuwa tumepiga hatua muhimu sana katika bara letu.
Cha Cha mboga mboga kinapaswa kuachia hii nchi maana wanauza nchi kwa maslahi ya matumbo Yao na sio umma wa Watanzania.
Alafu hawa wanao jiita mamlaka ya bandari toka lini wamekuwa wasemaji wa serikali ? Waache ujinga watanzania sio wapumbavu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.