Bandari: Shoka haliwezi kukata mti bila ya mpini

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,768
Reaction score
49,949
Kilichotokea juzi kuhusu bandari zetu, imenikumbusha maneno haya ya busara ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (tunamwomba Mungu mwema mjalie pumziko jema la milele).

Mwalimu Nyerere wakati anaongelea watu vibaraka walivyo hatari kwenye ustawi wa nchi, alisema kwamba shoka ambalo hukata miti, mpini wake ambao huwa unashikwa na mkataji miti, nao umetengebezwa kwa mti. Ukionesha kuwa kitakachotumaluza Watanganyika ni watanganyika wenzatu.

Shoka, japo limetengenezwa kwa chuma, lakini haliwezi kuukata mti bila ya mpini, na mpini huu umetengebezwa kwa mti pia.

Hivyo, hata mtu mbaya, akitaka kuwamaliza, aghalabu humtumia mwenzenu wa jamii yenu katika kukamilisha uovu wake. Huyu ndiye atakayeleta mafanikio katika maangamizi.

Jemedari Mkwawa, Wajerumani walipotaka kumvamia kwa mara ya kwanza, aliwamaliza wote. Alilimaliza jeshi lote la Mjerumani mpaka kamanda wao mkuu bwana Zelewski. Wote, askari wanaokadiriwa kuwa 100 waliuawa na kuzikwa kwenye kaburi moja.

Wajerumani baada ya kushindwa vibaya kwenye vita hiyo, kwa kiwango ambacho hawakutegemea, tena wale wahehe wakiwa hawana hata bunduki. Na sasa wakawa wameteka bunduki 100, waliamua kwenda Ujerumani na kufanya maandalizi ya miaka mitatu. Baada ya miaka mitatu, Wajerumani walikuwa tayari kwa vita, na kwa mara ya kwanza, mizinga iliingizwa bara la Afrika. Lakini, pamoja na hizo silaha nzito, bado waliona wasingeweza kushinda vita bila kuwapata vibaraka, yaani askari wasaliti wa Mkwawa.

Wakampata askari mmoja wa mkwawa, huyo aliijua mipango yote ya jeshi la Mkwawa. Wakati askari wa mkwawa wakiwa wamefanya zoezi la advance to contact ili mapigano yafanyike kabla maadui hawajafika kwenye ngome ya wahehe huko Kalenga, askari mwasi wa Mkwawa alilipitisha jeshi la mjerumani kwenye njia tofauti na ambayo ilikuwa inajulikana hao askari wa Wajerumani wangeitumia, na hivyo kuwakwepa askari wa Mkwawa.

Wakati askari wa Mkwawa wakiendelea kuwasubiria maadui, tayari maadui walikuwa kwenye eneo karibu na ngome ya wahehe, na mizinga yao wakiwa wameiweka eneo linaloitwa Tosamaganga. Wakaanza kuvurumisha makombora ya mizinga ambayo wahehe hawakujua hata ni kitu gani. Wakawa wanaulizana hicho ni kitu gani, wengine wakasema, 'vitosa maganga (wanarusha mawe), na kuna simulizi zinasema ndiyo ulikuwa mwanzo wa jina la Tosamaganga.

Kwa hiyo mafanikio ya wajerumani dhidi ya wahehe, yalitokana na msaada wa mhehe aliyewaasi.

Hii inatufundisha kuwa, mwenzenu mmoja aliyeasi, ni hatari kuliko hata askari 1,000 wa adui. Sawa na ilivyo mpini mmoja uliopo kwenye shoka, unalifanya shoka liangamize hata miti 1000 iliyosimama.

Na juzi imedhihirika wazi wabunge wachache waasi wa Watanganyika ni hatari kwa maslahi ya Taifa kuliko Wageni 1,000. Waliotumaliza siyo Waarabu wala Wazanzibari bali ni watanganyika waliotumika kuwaangamiza watanganyika kwa r7shwa ya fedha na magari. Hawa ndio waliotumika kuonesha kuwa watanganyika wote wameridhia.
 
Hili mbona lipo wazi muda mrefu sana mkuu Bams,adui wa Tanganyika ni watanganyika wenyewe.

Tunaishi na jamii ya kinafiki ambayo haija wahi tokea kiasi kwamba mpaka una shangaa hawa watu akili zao zipo timamu kisawa Sawa.
 
Kwa kweli Wazanzibari wametudharau sana. Walipima uduni wa akili na uelewa wa watu kama akina Musukuma, wakautambua uduni na ufinyu wa akili zao, wakaona wanaweza kutumika katika kuwaangamiza watabganyika wenzao.
 
Huyu Muasi ni Tulia, Lusinde na wenzao
 
Fatma Karume: Hakuna Mzanzibari aliyeuza Bandari ulizaneni wenyewe huko huko 🤣🤣

Hata Yesu alisalitiwa na ndugu yake Yuda Iskarioti aliyekuwa Mtunza Hazina
 
Kilichotokea juzi kuhusu bandari zetu, imenikumbusha maneno haya ya busara ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (tunamwomba Mungu mwema mjalie pumziko jema la milele).

Mwalimu Nyerere wakati anaongelea watu vibaraka walivyo hatari kwenye ustawi wa nchi, alisema kwamba shoka ambalo hukata miti, mpini wake ambao huwa unashikwa na mkataji miti, nao umetengebezwa kwa mti. Ukionesha kuwa kitakachotumaluza Watanganyika ni watanganyika wenzatu.

Shoka, japo limetengenezwa kwa chuma, lakini haliwezi kuukata mti bila ya mpini, na mpini huu umetengebezwa kwa mti pia.

Hivyo, hata mtu mbaya, akitaka kuwamaliza, aghalabu humtumia mwenzenu wa jamii yenu katika kukamilisha uovu wake. Huyu ndiye atakayeleta mafanikio katika maangamizi.

Jemedari Mkwawa, Wajerumani walipotaka kumvamia kwa mara ya kwanza, aliwamaliza wote. Alilimaliza jeshi lote la Mjerumani mpaka kamanda wao mkuu bwana Zelewski. Wote, askari wanaokadiriwa kuwa 100 waliuawa na kuzikwa kwenye kaburi moja.

Wajerumani baada ya kushindwa vibaya kwenye vita hiyo, kwa kiwango ambacho hawakutegemea, tena wale wahehe wakiwa hawana hata bunduki. Na sasa wakawa wameteka bunduki 100, waliamua kwenda Ujerumani na kufanya maandalizi ya miaka mitatu. Baada ya miaka mitatu, Wajerumani walikuwa tayari kwa vita, na kwa mara ya kwanza, mizinga iliingizwa bara la Afrika. Lakini, pamoja na hizo silaha nzito, bado waliona wasingeweza kushinda vita bila kuwapata vibaraka, yaani askari wasaliti wa Mkwawa.

Wakampata askari mmoja wa mkwawa, huyo aliijua mipango yote ya jeshi la Mkwawa. Wakati askari wa mkwawa wakiwa wamefanya zoezi la advance to contact ili mapigano yafanyike kabla maadui hawajafika kwenye ngome ya wahehe huko Kalenga, askari mwasi wa Mkwawa alilipitisha jeshi la mjerumani kwenye njia tofauti na ambayo ilikuwa inajulikana hao askari wa Wajerumani wangeitumia, na hivyo kuwakwepa askari wa Mkwawa.

Wakati askari wa Mkwawa wakiendelea kuwasubiria maadui, tayari maadui walikuwa kwenye eneo karibu na ngome ya wahehe, na mizinga yao wakiwa wameiweka eneo linaloitwa Tosamaganga. Wakaanza kuvurumisha makombora ya mizinga ambayo wahehe hawakujua hata ni kitu gani. Wakawa wanaulizana hicho ni kitu gani, wengine wakasema, 'vitosa maganga (wanarusha mawe), na kuna simulizi zinasema ndiyo ulikuwa mwanzo wa jina la Tosamaganga.

Kwa hiyo mafanikio ya wajerumani dhidi ya wahehe, yalitokana na msaada wa mhehe aliyewaasi.

Hii inatufundisha kuwa, mwenzenu mmoja aliyeasi, ni hatari kuliko hata askari 1,000 wa adui. Sawa na ilivyo mpini mmoja uliopo kwenye shoka, unalifanya shoka liangamize hata miti 1000 iliyosimama.

Na juzi imedhihirika wazi wabunge wachache waasi wa Watanganyika ni hatari kwa maslahi ya Taifa kuliko Wageni 1,000. Waliotumaliza siyo Waarabu wala Wazanzibari bali ni watanganyika waliotumika kuwaangamiza watanganyika kwa r7shwa ya fedha na magari. Hawa ndio waliotumika kuonesha kuwa watanganyika wote wameridhia.
Unatumia nguvu kubwa sana kupinga uwekezaji wa bandarini mpaka kuja na mifano ya Mkwawa na wahehe.

Sijui kama unaiona bandari yetu kwa mapana yake, sijui kama unaiona neema ya Mungu ya sisi kuwa na kilomita 1420 za fukwe kulinganisha na chache za Kenya!.

Sijui kama unaelewa maana ya Rwanda kuwa tayari wameshaijenga dry port kwa ajili ya mizigo ya bandari kavu inayokwenda kutumiwa na DP World.

Sidhani kama unaelewa ni kwanini trilioni 15 pesa nyingi sana imetumika katika kujenga reli ya SGR iliyoanza kujengwa 2016.

Mkuu hakuna namna ni lazima pale bandarini tuondokane na utendaji kazi ya kusaini makaratasi kwa mkono na twende katika dunia ya kidigitali.

Sijui kama unakutana na kero ya kusubiri wiki nzima mzigo wako ushushwe melini wakati kisasa na kisayansi ni kazi ya ndani ya saa 24 inakuwa imemalizika.
 
Back
Top Bottom