Sio QT ni PC ,QT ni mwanafunzi anayerudia masomo ya kidato cha pili,anapaswa kujisajili kama PC na asajili masomo mawili KEMIA NA FIZIKIA tu kupunguza mzigo kama BIOLOGY alifaulu aachane nayo atajiongezea mzigo,akifaulu ataunganisha namba zake kuomba chuo .
Hakuna Control number ya 30k ,unaomba control number kwa kila chuo unachoomba unalipia 10k ,ila ikishafikia 30k hapo utakuwa na uwezo wa kuongeza vyuo utavyotaka hadi 12 kwa iyo iyo 30k
Kujiajiri utajiajiri vipi?? ,Utafungua kiwanda au shule?? Iyo kozi ni lazima utafute ajira, Ajira zipo japo lazima CONNECTION sababu kuomba kazi viwandani bila SUPPORT sidhani kama unatoboa, kuna jamaa angu kaunganishwa na mtu saivi anakula maisha kiwanda cha MTIBWA SUGAR .
Kwa uzoefu wangu, shida iko chuoni na wala Sio nacte, mambo ya kukosa matokeo au namba ya mtihani ni ishu za chuo, kuna mawili ni uzembe wa chuo au ujuaji wa wanafunzi (UKIJIFANYA MJUAJI SANA CHUONI WALIMU WANAKUKOMOA TU ) ,namna ya kulitatua mkamshike mkono mwalimu mmoja kwa siri atawasaidia...
Utaratibu ni mrefu sana, iko hivi ,unatakiwa uende polisi ukatoe maelezo namna cheti kilivyopotea, wao watakupa fomu fulani, baada ya polisi unatakiwa utoe tangazo kwenye gazeti, baada ya hapo ingia Kwenye mfumo wa necta kuna sehemu ya kuomba cheti kipya, ukifika iyo sehemu watadai uwatumie ile...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.