Msaada: Nimeomba 'Control Number' NACTE ya kulipia 10,000 badala ya 30,000. Sifahamu namna ya ku-cancel nianze upya

gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
3,283
3,274
Salaam,

Wanabord ninaomba kufahamishwa kwa yeyote inaefahamu anisaidie kunifshamisha.

Nacte wamefungua dirisha la udahili kwa vyuo vya afya ambapo deadline ni mwisho wa mwezi huu.

Kwa kosa nililofanya la kupata control number ya 10,000 nitalazimika kuomba chuo kimoja tu hivyo nitakua na risk yakukosa nafasi.

Nimehangaika kupiga namba zao hawapokei.

Swali,je nifanyeje ni cancel hii control number ili nianze upya?
 
Lipia hiyo halafu utaweza ku-ADD na kuomba bill zingine, kama 30,000 ni kwa vyuo VITATU basi kila chuo kina bill yake…. endelea na mchakato mfumo utakuelekeza.
 
10,000 mpaka unafungua Uzi?
Hayo ni mawazo yako,
Inawezekana nikalipa na mfumo usiniruhusu kuanza upya,ninachohitaji ni maelekezo kwa anaefahamu,

Watoto mnaokaa kwa shemeji zenu huwa mnadharau sana.

Hata hivyo pesa haipaswi kudharauliwa.

Yoyo kwa yote nashukuru kwa mchango wako pia kwani umeifanya thread kuwepo
 
Jaribu kuomba control number ya hiyo 30k ukipata,hiyo 10k usilipie
 
Jibu: Unalipa 10k mara 3 yaani utatumia Control no 3 tofauti. Lipia 10k omba chuo, Omba C.No nyingine lipa tena Omba chuo na Rudia Process.
 
Wewe nenda kaAdd Choice chagua chuo wakati wa kusave choice watakuletea Option ya kuomba Control No. Fanya hivyo lipia kisha rudi Uconfirm Choice.
 
Hakuna Control number ya 30k ,unaomba control number kwa kila chuo unachoomba unalipia 10k ,ila ikishafikia 30k hapo utakuwa na uwezo wa kuongeza vyuo utavyotaka hadi 12 kwa iyo iyo 30k
 
Back
Top Bottom