Recent content by Bozi

  1. B

    Tozo za miamala ya simu ni kikwazo kwa biashara ndogo

    Bila shaka hufanyi biashara na wala hujawahi, mawazo yako ni nje ya muktadha.
  2. B

    Tozo za miamala ya simu ni kikwazo kwa biashara ndogo

    Kama kuna mahali serikali hii imekosea ni kuhusu hii tozo ya miamala ya simu, madhara yake yatakuwa makubwa sana kwa biashara za watu wa chini. Wafanyabiashara wadogo wengi hawatumii bank kufanya manunuzi na malipo mbalimbali. Tozo iliyowekwa ni kubwa kuliko faida tarajiwa katika muamala...
  3. B

    Kubakia madarakani kwa Mbowe na timu yake: CHADEMA jitokezeni mseme kama hakuna uchaguzi na hamna mbadala wa Mbowe

    Bwana Petero angeanza kutueleza, ni lini CCM ilishawahi kufanya uchaguzi wa mwenyekiti wake. Kiti cha mwenyekiti wa CCM ni cha rais yeyote atakayechaguliwa. hapo uchaguzi uko wapi? Sasa tofouti ya CHADEMA na CCM iko wapi, wote hawafanyi uchaguzi wa mwenyekiti wa chama.
  4. B

    Hii elimu bure ya Magufuli watoto wao wanasoma hizo shule za bure? Ndugu zao wanafundisha huko? Inatusaidia kimaendeleo? Inaendana na teknolojia?

    Acha hizo wewe, nani katika cooperate companies anashikilia cheo cha maana katoka Kayumba. Kayumba wanauwezo wa kukariri tuu. Nipe mifano mitatu au tano hapa. Halafu mie nikupe mifano mia hapa hapa bongo. Shule za serikali zina matatizo na product zake haziwezi kupambana nje ya TZ
  5. B

    Adhabu ya viboko ilijenga taifa lenye nidhamu kuanzia mashuleni mpaka majumbani !

    Viboko havimfanyi mtoto awe na nidham, vinamjengea uoga na kutojiamini. Ndio maana hata mtoa mada ana hofu hajiamini. Ni dhambi kubwa kumjengea uoga kijana mdogo kwasababu hatajiamini hata akiwa mtu mzima. Anakuwa tu bendera fuata upepo.
  6. B

    Kubakia madarakani kwa Mbowe na timu yake: CHADEMA jitokezeni mseme kama hakuna uchaguzi na hamna mbadala wa Mbowe

    Mimi nakubaliana na wanaodai uchaguzi ndani ya Chadema ufanyike kwa mujibu wa katiba,lakini uchaguzi ukifanyika Mbowe bado anatosha. Kule CCM mbona hakujawahi kufanyika uchaguzi, huwa wanapitisha tuu, yeyote atakayekuwa Rais basi lazima awe Mwenyekiti. Na sababu yao iko wazi, CCM bila dola ni...
  7. B

    Kama Tume ya Uchaguzi ( Nec) siyo huru kwanini wapinzani miaka yote wanakubali kushiriki uchaguzi

    Tanzania kuna vyama ambavyo havina diwani wala mtaa achilia mbali Mbunge, vimepigwa marufuku kueneza itikadi zao na kutafuta wanachama wapya kwa njia ya mikutano,mpaka pale uchaguzi utakapoitishwa, kwa maana nyingine vinaingia kwenye uchaguzi, 1. mosi, kujitambulishe vifahamike kama vipo 2...
  8. B

    Rais Magufuli amefanya kosa gani la kikatiba/kisheria hadi alaumiwe kuhusu misamaha ya wahujumu uchumi na mafisadi?

    Mselewa naye kiazi tuu, dishi limeyumba. Labda aseme anafanya masihara!
  9. B

    Profesa Kabudi Akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa: Tanzania tumedhamiria kubadili maisha ya watu, Azungumzia pia kuhusu Zimbabwe na DRC

    Mbona viti ukumbini viko wazi, bado tunasafari ndefu sana kujenga heshima yetu nje. Mbona big boys walipokuwa wanahutubia ukumbi ulikuwa umefurika. siku nyingine wawe wanatupanga mwanzoni au karibu na nchi kubwa tusikike na sisi. .
  10. B

    Ofisi za NSSF Mwanza na nyanyaso kwa wafanyakazi

    Hili liko nchi nzima, kwamba Rais alisema amesitisha sheria ya awali hivyo unaweza kuomba pesa yako, hesabu tu hukumuelewa vizuri. Hii sheria ni mbaya haikuzingatia mazingira ya ajira za Tanzania. Serikali na Bunge letu lilitunga sheria mbaya, hata kama hio pesa imepelekwa kwenye miradi ya...
  11. B

    Tunaofuatilia mafao NSSF tunateseka

    Watu wanateseka sana, NSSF inatesa watu jamani. Kazi huna, umezunguka kila mahali kutafuta kazi umekosa, hakuna kazi, umechoka ukaona acha nifikirie kufanya jambo lingine. Unaomba pesa zako unanyimwa, unasumbuliwa, unazungushwa,familia inateseka, watoto wanakosa shule, unakosa mwelekeo...
  12. B

    Tunaofuatilia mafao NSSF tunateseka

    Unaweza kusema aidha shirika halina hela kulipa mafao au haipo nia ya kulipa watu stahili zao. Ukifika ofisi za NSSF wafanyakazi wanachojua ni kukupiga tarehe tuu, wakidai kila kitu kinashughulikiwa makao makuu ya NSSF, ukisikia jambo lako linashughulikiwa DSM basi ni kama umeambiwa haulipwi...
  13. B

    NSSF inatutesa tuliopoteza ajira

    Hali ni tete kwa tuliopoteza ajira, maisha ni magumu familia zetu zinateseka sana. Kapesa kadogo kalikokuwa kanaenda NSSF kwa miaka na miaka nako huwezi kupewa. unatakiwa mpaka ufikishe umri wa miaka 60, ni mlima mrefu huo ukiwa huna kazi. Wanakuambia watakuwa wanakulipa 33% ya uliokuwa...
  14. B

    Mbunge Garisa: Tanzania Walituchomea kuku,wakapiga mnada ng'ombe wetu

    Ni rahisi tuu. wakenya wote walioko Tanzania warudi kwao na pia wa TZ walioko Kenya warudi TZ. Kisha tuone nani Kichaa zaidi
  15. B

    Jinsi ya Kusajili kampuni katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Nakuja kwenu kuomba msaada, nataka kusaji jina la biashara/kampuni katika website ya Brela ila napata changamoto kwani naishia hatua ya awali tuu ya kuingiza email na taarifa zangu kama namba za kitambulisho cha taifa. Nimekamilisha zoezi hili na kuambiwa kuwa taarifa zangu zimetumwa kikamilifu...
Back
Top Bottom