Mwakilishi mpya wa Jimbo la Bububu, Hussein Ibrahim Makungu, jana aliapishwa huku Mawaziri wa Chama cha Wananchi (CUF) na wajumbe wake wakisusia tukio hilo kwa kutoka nje ya ukumbi wa Baraza la Wawakilishi (BLW) Chukwani Zanzibar.
Makungu aliapishwa mbele ya Spika wa Baraza hilo, Pandu Ameir...