Hivi kweli kuna watu wanapiga hela online? Mimi naona kama uzushi tu!

Pain killer

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
14,193
21,335
Habari wakuu

Maisha kwa sasa yanaenda kasi sana, Sisi vijana katika harakati za kutafuta pesa tunakutana na changamoto nyingi sana ,sasa kuna hii njia inaitwa "kupiga hela online ,ukiwa na simu yako na bando " Mimi nimeshafanya uchunguzi sana online businesses wanazosema ni zipi hizo au ni hizi ...

Cryptocurrency (sarafu za kidigitali)..

Forex ..

Betting ..

Nyingine ni network marketing ,huku utakutana na website zinatokea na kucollapse watu wanapigwa hela ,ila kutwa status kupost eti wanapiga hela eg ,pamafund ,smarthela ,global alliance ,qnet ,forever living ....

Kuna mengine mengi yanaibuka na kutoweka kwa kweli mpaka nabaki mdomo wazi na watu wanaweka hela huko ,wanapigwa ,ila ni full kujipa moyo et wanapiga hela ,wanasema wanapiga hela wakiwa wamelala kitandani ....

Hawa watu wa online wanawaona wauza mihogo ,machinga ,wauza migahawa ,wauza matunda ,chips ,washona viatu ,wapiga debe ,....hao wote wanawaona kama hawana akili ya kutafuta hela ,ila wao ndio wanajua hahaaaaaa....

Kusema kweli kama online business watu wanazosema ndio hizo hapo juu ,sina budi kusema kuwa ,watu wanaofanya hayo mavitu ni wavivu wa kufikili na "HAWATAKUJA KUFANIKIWA MPAKA MWISHO WA DUNIA"...

Yaani wanapigwa pesa mpaka akili ziwakae sawa, ..

Hakuna pesa za bure online, Fanya kazi kwa bidii, jitume, ndio njia ya kupata pesa ..

Forex ingekuwa biashara, serikali ingechukua $100,000 ikawaintrade na kutengeneza pesa ,...

Sarafu za kidigital zingekuwaa deal, hakuna tajiri ambaye angepoteza pesa kufungua kiwanda ,kulipa wafanya kazi, kodi, aridhi, na mabilion ya pesa wakati angeweza kununua hizo sarafu ..

Mh Raisi naamini atashauriwa vizur kuhusu hizo sarafu ..

Vijana tokeni nje, mkafanye kazi, ardhi ipo, mashamba yapo, mbegu zipo, hizo smart phone zinawadanganya, hakuna pesa utaingiza umelala kitandani ....

Uzi tayari
 
Na mtazamo tofauti kidogo na wewe,binafsi na deal na fx pamoja na index.
Kama vile biashara nyingine zilivyo LOSS ni kitu cha kawaida ila kikubwa unahitaji kuinvest kwenye knowledge sana ili kuminimize loss na kuongeza profit.
Sio kitu ya kujifunza usiku mmoja kesho uamke kama ref wayne it takes time and a lot of effort.
 
Yaaah that is forex ,bora umeelezea pande zote mbili ....

Kuna watu ukikutana nao wao ni full kudanganya ,wanapigaa hela ,wamejenga nyumba ...
 
Fulani akipiga hela / pesa haimaanishi kwamba jambo ni viable au sustainable..., Hata DESI / Pyramid Schemes AKA PONZI Schemes kuna watu walipiga pesa ila in the end watu walilia....

As a Country hatuwezi kutegemea bahati / kubahatisha kama njia ya kuwaondoa majority katika extreme poverty..., ni kuongeza stress na magonjwa ya akili ambayo eventually kama taifa / jamii tutagharamikia...
 
Noted
 
Mkuu hii njia ya online kupiga hela ,kwamba ndio njia ya kujiajiri ,mimi huwa nabaki mdomo wazi ,kwani mambo yote ya online ni almost gambling ...

Sijui huwa wanakuwa wanatushawishi kubet ...
 
kwa uzoefu wangu online business inayolipa ni zile za aina ya upwork, affiliates na hizi za contents writing, hizo kweli zinalipa ial nyingine siziamini
Yaaah kama ni hizi ,basi hela ipo ....

But mimi nafuatilia rafiki zangu wote kutwa status wanajimwambafi wanafanya online business ....

Fuatilia sasa uone ,utasikia forex,smart hela ,pamafund ....

Daa unabaki unashangaa ....
 
Hahahah hizo hata mimi siziamini, nitakomaa na nyingine lakini si hizo
 
Taja online busines tofauti na nilizotaja hapo juu ....

Mkuu tafadhari naomba unitajia hizo online business tofauti na hayo makundi nimeyoweka hapo juuu ...
Kwa uzoefu wangu online business inayolipa ni zile za aina ya upwork, affiliates na hizi za contents writing, hizo kweli zinalipa ial nyingine siziamini
 
Kuna freelancing service kama fiverr, google adsense, linkedin na publishing za contents hasa miziki
Hizo zote hazina hela ,na huwezi kutengeneza pesa kiasi cha kununua gari au kujenga nyumba kama wanavotuaminisha mtaani kuwa kupita online business basi huna haja ya kutafuta kazi ....!
 
Back
Top Bottom