Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,770
- 46,480
Usimlaze mtoto na wageni au ndugu wowote wa kiume ambao ni wakubwa kwake.
Usimtoboe masikio akiwa mdogo, muache aje kutoboa kwa hiari yake.
Usimfunge hirizi au kitovu mkononi, shingoni au kiuononi.Hiyo ni mizigo ya uchafu tu kwake, unaweza kuvaa wewe mzazi wake badala yake kama unazihusudu sana.
Usimlazimishe kwenda madrasa, msikitini au kanisani, akifikia umri wa kuchagua mwenyewe ataamua wapi pa kwenda.
Usimvalishe pia hijabu, kwa maeneo yenye joto kama Morogoro ni mateso makubwa sana.
Usimpake wanja mtoto mdogo anapendeza bila hayo makorokoro, kama ni kumkinga na jicho baya huo nao bado ni ushamba.Pia usimsuke nywele za kumtesa au kumnyoa viduku.
Usimuonjeshe pombe.
Akiwa anakataa kwenda shule au afurahii shule yake chunguza sababu ni zipi.
Usipende kuchapa mtoto msumbufu kuna watoto wenye matatizo ya Attention deficit hyperactivity disorder (ADHD), Dyslexia au autism
Usitumie viboko au vipigo kama njia kuu ya kumfundisha adabu au kutatua matatizo ya mtoto.Hii ikiwezekana acha nayo kabisa.