Hatimaye nimepata wa kunituliza, hivi sasa mimi ni "Miminimama wa Tajiri"

miminimama

JF-Expert Member
Aug 2, 2018
691
1,780
Sijui niandike nini.

Lakini ni kuwa nina mpenzi ananipenda nami nampenda. Huyu mtu alikuwa ni mwanaume wa ndoto yangu. Nimepata mwanaume yule yule niliyekuwa nammpicture.

Hello tajiri wangu G unajua vile nakupenda. Nawewe tupende hivi hivi kila siku. Ahsante kwa kila kitu maana ni vingi mno. Upendo wako kwetu ni wa hali ya juu.

Ile sentensi ya kuwa "....hii ikisimama hutokuwa na wasiwasi na future ya mtoto..." ilimaanisha vitu vingi sana.

Nakupenda nakupenda nakupenda.

Wengi mtajiuliza huyu dada ni nani?Miminimama ni yule niliyekuwa naandika humu natafuta mume.
Nimepata zaidi ya mume.

Lakini haikuwa safari ya muda mfupi. Ni safari ya miaka 2 humu. Humu ndani kuna watu wa aina zote umakini na kutokata tamaa unahitajika.

Kabla ya kuwa "single mom" nilikuwa mwanamke mwenye maono yangu, mfano bora kwa kila mzazi mwenye bint. Lakini safari yangu ya kuwa mama ilibadilisha kila kitu kwenye maisha yangu. Nilipitia magumu mengi sana.

Mwenyewe G wangu ananiambia unaweza kumpata mwandishi mzuri akaandika vizuri hayo mapito na nikatengeneza pesa.

Miaka 6 kwangu ni kilio tu na majonzi. Hata wale watu wa karibu yangu ambae wangenipa moyo na ushauri wote waligeuka.

Nilikuwa mimi na mwanangu tu. Embu fikiria hii mtoto anaumwa unamtumia msg baba wa mtoto kuwa anaumwa hakujibu kupiga simu anajibu sina hela. Lakini just a stranger anakupelekea mtoto hospital, anampeleka shule tena si shule tu ni shule bora kabisa.

Maisha yalikuwa tofauti na magumu mno kabla kumpata huyu mwanaume. Just two of us mimi na mwanangu.

No happiness.
No career.
No food.
No shelter.
No clothes.
No money.
No love.

Yaani kila kitu ni negative. Lakini boom unampata mwanaume ambae anakupa kila kitu na kila kitu kinakuwa kwenye mstari huyu mwanaume ameenda mbali mno na ninajivunia sana na kila siku naomba Mungu amtunze na amlinde.

Ampe umri mrefu. Kwangu sasa hivi Kuna furaha. Mtoto wa single mom amepata baba. "Ninasemelewa kwa baba" siku hizi.

Ninafuraha ya maisha, ni mdada ambae G ananijenga kuwa tajiri si kwamba yeye ni tajiri wa Mali hapana. Yeye ni tajiri wa moyo ana upendo sana.

Pale nilipoishia miaka 6 nyuma yeye ndo anapoanzia. Mwanaume anayenipa vingiiiiiiiiiiiiiiiiii na vizuri mno. Ameituliza akili yangu,amenituliza kitandani amenituliza na mfukoni .

Hili ni penzi ambalo nimelisotea miaka mingi sana kulipata. Nitalitunza na kulienzi siku zote. Nawaombea wote ambao humu mnatafuta wapenzi kwa dhati mpate.

Ahsante G, ahsante kwa kunionyesha mimi ni mwanamke wa pekee kwako. Ahsante kwa upendo wako kwetu. Ahsante kwa kutukumbatia. Ahsante kwa kurudisha tabasamu na nuru kwangu. Ahsante kwa kunifuta machozi. Ahsante kwa kunitengeneza niwe mwanamke wa kipekee na kurudisha ndoto zangu.

Ahsante kwa kuwa nami kwenye kila ninalopitia. Ahsante kwa penzi lako ni tamu mno. Ahsante kwa best love making unanifanya nitake mara kwa mara. Ahsante kwa kunifanya niwashwe mda wote. Ahsante kwa kunikuna mda wote kila nikiwashwa.

Ahsante kwa kuniongoza ahsante kwa ubongo wako maana unafanya kazi mno kwa ajili yangu. Ahsante kwa pesa zako zote unazonipa na unazoendelea kunipa kila siku nakuombea ubarikiwe zaidi na zaidi na uwe tajiri Kama ulivyo moyo wako. Ahsante kwa kunilinda. Ahsante kwa kila kitu baba K wangu .

Nakupenda mno. Mimi ni wako mpaka kifo kitutenganishe.


Update.
Mwaka sasa mimi na yeye penzi limetaradadiiiiii imebaki history, sijawahi kulia, kuwa na huzuni wala kujuta kukujuana nae.

Na kama kuna maisha baada ya hapa ninaomba pia niwe na G wangu.

Nakupenda babaaaa
 
Mwanzo 3:16
Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.

Yaani tukiwaambia humu utukufu wa mwanamke ni kwa mwanaume na ndipo ilipo furaha ya kweli ya mwanamke cariha anasema mfumo dume.

Hongera kwa kumpata Baba yako mheshimu na uyalinde maono yake
 
Naamini siku yangu itaenda poa kwa kukutana na uzi huu asubuhi hii,

Hongera sana best yangu kwa kupata kile moyo wako unapenda, ukamtunze, ukamuheshimu, ukambeleze mwanaume wako, wanaume aina hiyo hawapatikani kwa dunia hi tuliyomo, nimefurahi sana pamoja na wewe,

Kawe mwaminifu kwa gharama yoyote ile, hata ukiomba chochote kwa muumba wako utakipata Tena kwa wakati, usikubali kulala pasipo kusawazisha mgogoro wowote wewe na G, hata uwe ni mdogo vipi, jinyenyekeze kwake na kwa hakika kifo ndo kitawatenganisha

Kila la heri kwenu
 
Mama G anahitaji baby shower kwakweli...

Am happy for you my dear..Mungu wetu azidi kuwalinda na mzeeke pamoja wallah..

Hivi G ana kaka ake ?
Ana cousin wake.
Ahsante mpenzi nakumbuka ulikuwa unaniuliza kama kweli au natania.
Nilikuwa namaanisha na Mungu akanipendelea akanipa zaidi ya nilichoomba.
Kuna watu tunakutanishwa nao kwa sababu maalum.
Natamani uone jinsi mwanangu alivyo na furaha.
 
Naamini siku yangu itaenda poa kwa kukutana na uzi huu asubuhi hii,

Hongera sana best yangu kwa kupata kile moyo wako unapenda, ukamtunze, ukamuheshimu, ukambeleze mwanaume wako, wanaume aina hiyo hawapatikani kwa dunia hi tuliyomo, nimefurahi sana pamoja na wewe,

Kawe mwaminifu kwa gharama yoyote ile, hata ukiomba chochote kwa muumba wako utakipata Tena kwa wakati, usikubali kulala pasipo kusawazisha mgogoro wowote wewe na G, hata uwe ni mdogo vipi, jinyenyekeze kwake na kwa hakika kifo ndo kitawatenganisha

Kila la heri kwenu
Mpaka nimelia rafiki yangu.
Sijawahi kukutana na mahusiano ya aina hii.
Nazingatia huu ushauri.
 
Uzi nyingine ni za kutufanya tujiskie vibaya, au tujisikie hatuna bahati.btw hongera sana.

Mpelekee mama yake zawadi mwambie "asante mama kunizalia mme mwema"
Usijiskie vibaya Kuna wakati ukifika unakuwa wakati wa furaha mda wote.
Mimi nilimuuliza kuwa "hii furaha itakuwa siku zote au kwa mda mfupi?"
Jibu lake ni milele.
Nisiogope kujiachia kwake.
 
Mwanzo 3:16
Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.
Yaani tukiwaambia humu utukufu wa mwanamke ni kwa mwanaume na ndipo ilipo furaha ya kweli ya mwanamke cariha anasema mfumo dume.
Hongera kwa kumpata Baba yako mheshimu na uyalinde maono yake
Ahsante.
Lakini nafikiri mnamuelewa vibaya cariha
 
Back
Top Bottom