Arusha: Maduka yote ya kubadilishia fedha za kigeni(Forex) yasimamiwa na JWTZ, wananchi watakiwa kwenda Benki Kuu

Pozzers

JF-Expert Member
Sep 14, 2013
336
560
Maduka ya kubadilisha fedha za kigeni Arusha karibu yote yako chini ya ulinzi wa wanajeshi wakiwa na mitutu kwa kile kinachoitwa operation.

Its truly happening in Arusha.

--------
Ulinzi mkali umeimarishwa kwenye maduka karibu yote yanayohusika na biashara ya kubadilisha fedha(Forex)

Yadaiwa kuna oparesheni maalum inayoendelea ambayo hadi sasa haijafahamika inahusu nini

Aidha, wanaotaka kubadili fedha watakiwa kwenda kupata huduma hiyo Benki Kuu

F3.PNG
F1.PNG
F2.PNG


F4.jpeg

UPDATES;

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT)Profesa Luoga amethibitisha kuwa oparesheni ya kufanya ukaguzi katika baadhi ya maduka ya kubadilishia fedha jijini Arusha iliendeshwa na Benki yake kwa kushirikisha vyombo mbalimbali vya dola ili kubaini watuhumiwa wa uhalifu wa kutakatisha fedha.


Habari zaidi, soma=>Benki Kuu(BoT) yasitisha leseni za maduka ya kubadilishia fedha za kigeni Tanzania - JamiiForums
 
Habari zilizotufikia kituo hiki cha Mwanahabari huku kutokea Jijini Arusha zinasema kuanzia leo maduka yote ya kubadilisha fedha zote za Kigeni yatakuwa yanasimamiwa na JWTZ na wananchi wanatakiwa kwenda kubadili pesa zao Benki Kuu (BOT).

Baada ya mwakilishi wa Mwanahabari huru aliyepo Jijini Arusha kuhoji kwa Moja ya Mwanajeshi aliyekata asitajwe jina lake amesema ni amri kutoka juu zinazosema kuna utoroshaji wa pesa nyingi za kigeni.
 
Maamuzi ya ajabu sana haya!!

Haya ndio madhara ya kucheza na uchumi na sasa wanatumia jeshi badala ya weledi kurekebisha mambo!!

Kama shilingi inaporomoka, hiyo sio solution bali ni kuongeza tatizo.

Inawezekana kabisa wafanyabiashara wameona hali ni ya wasiwasi(shilingi yetu inayumba) hivyo ni bora wabadili fedha za kitanzania wapate hard currency (dola.n.k) ili kulinda mitaji yao.

Na demand ya dola ikiongezeka, maana yake shilingi itazidi kuporomoka huku dola ikizidi kupanda na hii huenda ndio hofu ya serikali.

Ni wazi tumeanza kuvuna tulichopanda.

Muda utasema ukweli ni upi.
 
Habari zilizotufikia kituo hiki cha Mwanahabari huku kutokea Jijini Arusha zinasema kwanzia Leo Maduka Yote yakubadilisha fedha zote za Kigeni yatakua yanasimamiwa na JWTZ na wananchi wanatakiwa kwenda kubadili pesa zao Bank kuu (BOT). Baada ya Mwakilishi wa Mwanahabari huru aliyepo Jijini Harusha kuhoji kwa Moja ya Mwanajeshi aliyekata asitajwe jina lake amesema ni amri kutokea juu zinazosema kuna utoroshaji wa pesa nyingi za kigeni
Hata kama pesa zinakwenda nje au kutoroshwa kwani zimebwa au ni majasho ya wenye pesa? Haka kanchi pathetic sana!
 
Maamuzi ya ajabu sana haya!!

Haya ndio madhara ya kuvuruga uchumi na sasa wanatumia jeshi badala ya weledi kurekebisha mambo!!

Kama shilingi inaporomoka, hiyo sio solution bali ni kuongeza tatizo.

Tumekosa maarifa!!

Tuache visingizio!

Wacheni dunia itutenge!
sasa hivi kila kitu ni jeshi tu
ni kama utawala wa kijeshi na tofauti ni kwamba mkuu wa majeshi haishi state house
Awamu hii kila mpiga deal atapiga goti kwa Magufuli..nchi hio inanyoka
 
Hatua nzuri

Wengi hawajui yanayotendeka..

Tena wangefanya watu wabadili kupitia akaunti zao za benki.. pesa inaingizwa na kutolewa ikiwa imebadilishwa kama hautoi kwenye akaunti

Inafanyika sana huko kwa nchi zilizoendelea..

Na watalii wakienda kubadilisha na passport zao zinaangaliwa kuonyesha... na kuwekewa rekodi..
 
Anyway, Nafikiri hii nchi ina shida kubwa sana kiuongozi na au kiongozi hana uwezo na ndo mwenye shida. Kama haya ndo mazingira wezeshi kwa ajili ya biashara Tanzania basi tutarajie hizo bureau de changes zote kufungwa na kodi waliokuwa wakilipa kupotea. Kuongoza nchi kwa mihemuko ni dalili za kushindwa!
 
Habari zilizotufikia kituo hiki cha Mwanahabari huku kutokea Jijini Arusha zinasema kwanzia Leo Maduka Yote yakubadilisha fedha zote za Kigeni yatakua yanasimamiwa na JWTZ na wananchi wanatakiwa kwenda kubadili pesa zao Bank kuu (BOT). Baada ya Mwakilishi wa Mwanahabari huru aliyepo Jijini Harusha kuhoji kwa Moja ya Mwanajeshi aliyekata asitajwe jina lake amesema ni amri kutokea juu zinazosema kuna utoroshaji wa pesa nyingi za kigeni


Nchi imemshinda....
 
Back
Top Bottom